Namibia’s President who is also the President of the ruling SWAPO’s party welcomes the CCM Chairman, President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete to Windhoek State House for the one day summit of Leaders of the Former Liberation movements in Southern Africa yesterday.
The CCM Chairman,President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete(right),SWAPO’s President Hifikepunye Pohamba(Centre) and ZANU PF President, Robert Mugabe meet at Windhoek State House in Namibia during the summit of Leaders of the Former liberation movements in southern Africa held yesterday.
Namibia’s President Hifikepunye Pohamba who is also the president of SWAPO’s ruling party,(right) delivers his opening remarks during the opening session of the one day summit of Leaders of former Liberation movements in Southern Africa held yesterday at Windhoek State House. From left, CCM’s Secretary General Wilson Mukama, CCM’s Chairman President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, ZANU PF Secretary General Didymus Mutasa and Zimbabwe’s ZANU PF president,Robert Mugabe.(photos by Freddy Maro).
Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa vilivoshiriki katika Ukombozi Kusini mwa Afrika, umekubaliana kuweka kumbukumbu na kuhifadhi yaliyokuwa maeneo yao makuu yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi.
Vyama hivyo vimekutana mjini Windhoek, Namibia tarehe 11 Agosti, 2011 chini ya uenyekiti wa Rais wa Namibia, Dr. Hifikepunye Pohamba ambaye pia ni Rais wa Chama kinachotawala cha SWAPO.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ameshiriki na kuelezea kuunga mkono uamuzi huo wa kuainisha maeneo hayo muhimu ambayo mengi yako nchini Tanzania kutokana na mchango wake mkubwa katika ukombozi wa bara la Afrika.
« Tumekubaliana kila Chama kiainishe na kuyatambua maeneo yake muhimu kwa ajili ya kulihifadhi kama kumbukumbu na historia ya nchi hizi, ambapo Tanzania tutasaidia katika kuyatambua lakini suala la kuyagharamia itakua jukumu la nchi husika ». Rais amesema.
Nchini Tanzania maeneo ya historia ya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika yako katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ikiwemo Chunya, Kongwa, Morogoro na Nachingwea.
Vyama vingine vilivyoshiriki katika mkutano huo wa viongozi ni Chama cha ZANU-PF kikiongozwa na Katibu wake Mkuu wa Kwanza ambaye pia ni Rais wa Zimbabwe, Rais Robert Mugabe, Chama cha MPLA, kimewakilishwa na Makamu wa Rais wa chama hicho Ndugu Robert De Almeida akimwakilisha Rais wa MPLA ambaye pia ni Rais wa Angola Rais Jose Eduardo Dos Santos.
Chama cha ANC kikiwakilishwa na Katibu Mkuu wake Ndugu Gwede Mantashe, ambaye amemwakilisha Rais wa ANC ambaye pia ni Rais wa Afrika ya Kusini, Rais Jacob Zuma na FRELIMO chini ya Katibu wake Mkuu Ndugu Filipe Paunde akimwakilisha Rais wa FRELIMO ambaye pia ni Rais wa Msumbiji Rais Armando Guebuza.
Pamoja na mambo mengine vyama hivi vimekutana kwa nia ya kuimarisha mahusiano baina ya vyama hivi ambavyo vina historia kubwa na muhimu sana katika Nchi za Kusini mwa Afrika.
Rais Kikwete na ujumbe wake wamerejea Dar-Es-salaam jana jioni (11 Agosti, 2011) mara baada ya kikao hicho cha siku moja kukamilika
MWISHO
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Windhoek, Namibia
11 Agosti, 2011
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...