Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dar es salaam mara baada ya kusaini msaada wa shilingi bilioni 40 kutoka Serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia miradi miwili ya maendeleo. Mradi wa kwanza ni ujenzi wa daraja la Rusumo lilopo mpakani wa Tanzania na Rwanda na uimarishaji wa barabara jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Hiroshi Nakagawa.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam
Home
Unlabelled
Serikali ya Japan yaipa msaada wa sh. bil 40 Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia miradi miwili ya maendeleo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hapa ndipo bongo panaponichanganya-bongo tambarare!
ReplyDeleteTunakusanya mapesa kutoka idara mbalimbali ili kuhonga kamati za bunge kupitisha bajeti ya wizara,kumbe bajeti zenyewe tunategemea kupewa misaada( serikali haina pesa).
Na ukiangalia bajeti nyingi ndani yake kuna pesa za vikao na training zinazofanyika kwenye mahoteli ya kitalii badala ya kutumia majengo ya serikali,na gharama nyingine ambazo sisi wananchi hatuzijui.
Sasa kwanini tusiombe bajeti za kweli(zisizokuwa na uchakachuaji) kupunguza gharama ili hiyo misaada itumike kwenye miradi inayokusudiwa ya kuleta maendeleo?
Hivi tutafika kweli?je hawa wanaotusadia hawatachoka?nadhani wao wanafanya kazi kwa bidii na maarifa na ndio maana wapo hapo walipo.
Eee bwana mungu tusaidie na hii nchi.
Naona tuanze na barabara za Dar maana foleni zimezidi, foleni ambazo zinadumisha maendeleo, hilo daraja halina haraka kwa sasa.Kwanini tusiwe kama Dubai au mamtoni?Tz tuna kila kitu .
ReplyDeleteTuwe na barabaran zile za juu na chini(Flying Over,Overpass and Underpass Roads) maana Dar kumejaa mijengo na pia tuwe na Toll plaza-Tollway/Toll Road kwa wale wenye haraka na wenye pesa za kulipia ili turudishe mkopo mapema.
Hili linawezekana kabisa na wala sio maajabu ila kwa bongo vigogo ndio watakapomalizia mijengo yao huko mbezi.
sema miradi gani huyo kasha punguza kwanza chake
ReplyDeleteYaani kweli wenzetu wameendelea sana.... Hawa jamaa si wamepigwa na kimbuga juzi tu? Badala ya sisi ndo tuwape misaada wao ndo wanatupa!!! Kweli bongo tegemeziiii...
ReplyDeleteSisi tunawasaidia akina nani?????