Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) limepiga marufuku kwa wachezaji wote ambao sio waajiriwa maarufu kama mamluki kushiriki kwenye michezo ya shirikisho hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa SHIMMUTA Award Safari, hatua kali zitachukuliwa dhidi ya timu yoyote itakayobainika kupeleka wachezaji wasio waajiliwa ikiwa ni pamoja na timu husika kuondolewa kwenye mashindano.

“Ikibainika kuwa kuna timu ya Shirika au Taasisi yoyote ambayo imeleta wachezaji mamluki kwenye mashindano, kwakweli hatutaifumbia macho na lazima timu hiyo tuiondoe kwenye mashindano,” amefafanua Safari.

Safari amesema michezo ya 42 ya shirikisho hilo inatarajiwa kufanyika mjini Tanga kuanzia tarehe 1 - 12 Oktoba, mwaka huu.

“Mpaka sasa jumla ya timu 37 za Mashirika ya umma, Taasisi na Makampuni binafsi hapa nchini tayari tumeshazipelekea barua za mwaliko wa kushiriki kwenye michezo hiyo”, ameongeza Safari.

Aidha jumla ya timu 4 ambazo ni pamoja na timu ya shirika la taifa la biashara, shirika la bandari, tembo hoteli na serena hoteli kutoka Tanzania visiwani - Zanzibar zimealikwa kushiriki katika michezo hiyo.

Safari ametaja michezo mbalimbali itayochezwa katika mashindano hayo kuwa ni mpira wa miguu, netiboli, vishale, kukimbia na gunia psmoja na kuvuta kamba. Michezo mingine ni bao, kalata, drafti, na kufukuza kuku.

Mwaka jana michezo ya SHIMMUTA ilifanyika jijini arusha ambapo shirika la TTPL liliibuka mshindi kwenye mpira wa miguu wakati timu ya netiboli ya CDA ilikuwa bingwa kwenye mchezo huo na shirika la utangazaji Tanzania lilishinda kwenye mchezo wa kuvuta kamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...