Kaka mimi ni mdau wa damu wa Blog ya Jamii,
Nimeona hii kitu huku Sauzi, nikasema ngoja nikutupie uwawekee wabongo wenzangu. Ni mambo ya alama za barabarani. Hapa wanakwenda hadi spidi 120. Na hata "TOCHI" za askari zinafahamika wapi zipo kwani kuna alama maalum kama unavyoweza jionea. Sie huko naona njia nzima toka Dar hadi Arusha spidi moja tu ama?
Mdau,
John Gabriel.
Eastern Cape, South Africa.
Nimeona hii kitu huku Sauzi, nikasema ngoja nikutupie uwawekee wabongo wenzangu. Ni mambo ya alama za barabarani. Hapa wanakwenda hadi spidi 120. Na hata "TOCHI" za askari zinafahamika wapi zipo kwani kuna alama maalum kama unavyoweza jionea. Sie huko naona njia nzima toka Dar hadi Arusha spidi moja tu ama?
Mdau,
John Gabriel.
Eastern Cape, South Africa.
Wsewe unacheza wewe huku kwetu jamaa trafiki wanakaa vichakani! wanajificha kwenye msitu mnene halafu wanakuchungulia kama unaspidi 100 badala ya 80 wakikuona mbiooooooooooo! na tochi zao kama kombolela. Bongo noma!
ReplyDeleteMdau umekosea. Barabara zetu pia zina alama. alama zinazooneshwa ni pale unapotakiwa kuendesha mwendokasi mdogo. kwa mfano labda unaingia sehemu yenye watu wengi utaonaumewekewa kibao cha 50 au kama kuna daraja n.k utaona wameweka kibao cha 30. Hiyo ya 120 kwa barabara zetu hakuna mahali wanapolazimisha kufanya hivyo kama wafanyavyo nchi nyingine. Kama hakuna vibao nivyotaja hapo juu ina maana unaweza kwenda mwendo wowote unaotaka, ila kwa mabasi ya abiria nadhani hutakiwi kuvuka 80 p.h. wadau wengine watasaidia.
ReplyDeleteSwaumu njema.
Mdau wa Mbezi Louis
si kwetu kuna alama za kuonyesha kama kuna kona au mtelemko au matuta mbele. Kuhusu speed ni hiyohiyo.
ReplyDeleteAlama kama mbele kuna tochi-camera hawawezi kuiweka, sasa Trafiki watakula wapi? Trafiki polisi uwa wanajificha vichakana, then kafla bib vuu wanajitokeza barabarani na tochi, yatakayotokea hapo mungu anajua
Sio kweli Gabriel kwamba bongo hadi arusha au mikoa mingine ni spidi moja tu. Tafiti zaidi, kuna hadi 20 na 30, hasa unapoingia katika miji au vitongoji.
ReplyDelete"Sie huko naona njia nzima toka Dar hadi Arusha spidi moja tu ama?" Mdau huna hata uhakika na unachouliza...au wewe hujakaa Bongo? Bongo pia zipo hizo alama! Wewe endelea kusafisha macho na kutoa ushamba maana hujawahi kuwa nje ya nchi, na wala hujatembea tz uone nchi yetu ilivyo. Nani alikuambia Bongo hakuna Alama za Barabarani? Alama zipo, kwa taarifa yako hizo alama zote ulizoonyesha hapo zinatumika nje ya mji na sio katikati ya mji! kama umewahi kusomea udereva ungezijua hizo alama toka awali. Sema kilichopo hapa kwetu ni uvunjaji wa sheria na kutokuzingatia masharti ya udereva bora. Eti "ngoja nikutupie wabongo wenzangu" acha dharau zako za kishamba!..kalagabaho!..lete kitu kingine na wala sio hicho!
ReplyDeleteAlama zipo huku Bongo,ila zaidi kilichokosekana kutoka ktk hiyo picha yako kwa hapa Bongo ni hiyo alama ya Tochi,na kwa balabala ya Dar - Mtara
ReplyDeletekuna alama za 100 speed ambavyo kwaiyo ya Dar - Arusha mwisho 80 kulingana na wingi wa magari lakini si kwamba ipo alama moja tu!!
Mdau wa Mbagala.
Ama kwa hakika mamlaka husika hazifanyi kazi stahiki katika kuhakikisha kuwa alama za msingi zinakuwepo ktk barabara. Japo kwa uchache sasa kuna ongezeko la alama hizo ukilinganisha na ilivyokuwa hapo awali.
ReplyDeleteMfano mzuri ni barabara kadhaa za katikati ya mji Dar zimefanywa kuwa barabara za njia moja (One Way) lakini cha kushangaza ni kuwa hakuna alama zozote katika barabara hizo zinazoashiria hivyo.
Sidhani kama kuweka alama hizi ni ghali kiasi cha kusema mamlaka husika haziwezi kuzihimili. Ila nadhani ni uzembe na kutokujali kwa wahusika.
Kama tunashindwa katika vitu vidogo kama kuhakikisha barabara zetu zina alama stahiki, sidhani kama tutaweza kuhakikisha usalama barabarani. Ni kweli madereva wengi wanaendesha bila kuheshimu sheria barabarani, ila sijui ni kwa namna gani tunaweza kumchukulia hatua dereva mvunja sheria hali ya kuwa alama zinazoashiria sheria au utaratibu wa uendeshaji salama barabarani hazipo!
Mdau Kigonsera.