MECHI YA NGAO YA JAMII (COMMUNITY SHIELD)

Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya mabingwa watetezi Yanga na Makamu Bingwa Simba itachezwa usiku (Agosti 17 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Boniface Wambura
Afisa Habari TFF
Uamuzi wa mechi hiyo kuchezwa kuanzia saa 2.00 usiku umetokana na sababu kadhaa, kubwa zikiwa mbili; Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na pia Agosti 17 mwaka huu kuwa ni siku ya kazi.
Pambano hilo litatanguliwa na mechi ya vikosi vya pili (U20) vya timu hizo ambayo yenyewe itaanza saa 10.30 jioni. Mechi ya Ngao ya Jamii baada ya dakika 90 kama mshindi hatapatikana, zitaongezwa dakika 30. Katika muda huo nao kama mshindi atakuwa bado hajapatikana, itatumika mikwaju ya penalti.
Mechi hiyo imepata mwekezaji (Big Bon) na hivi sasa wadau wake wakuu- Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu husika ziko katika mazungumzo ya mwisho mwekezaji huyo. Kwa redio ambazo zinataka kutangaza mechi hiyo moja kwa moja zinatakiwa kuwasiliana na Idara ya Habari na Mawasiliano ya TFF ili kupewa masharti ya kufanya hivyo.
Pia unafanyika utaratibu wa kuuzwa futari uwanjani mara baada ya mechi ya vikosi vya pili ili kuwawezesha washabiki waliofunga kutohangaika kutafuta sehemu ya kufuturu.


Kwa Habari zaidi toka TFF
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mbwegelembwegeleAugust 12, 2011

    Hivi hatuna uwezo kwa kubuni vitu vyetu wenyewe. Tunacopy kila kitu.

    Community shield ???
    'The Football Association Community Shield (formerly the Charity Shield) is English football's annual match contested between the champions of the previous Premier League season and the holders of the FA Cup at Wembley Stadium. If the Premier League champions also won the FA Cup then the league runners-up provide the opposition. Often seen as a "glorified friendly" which ranks below the FA Cup and League Cup, the fixture is a recognised football Super Cup. Organised by the Football Association, proceeds from the game are distributed to community-based initiatives and charities around the country. Revenue from the gate receipts and match programme sales is distributed to the 124 clubs who competed in The FA Cup from the First Round onwards, for onward distribution to charities and projects of their choice, while the remainder is distributed to the FA's national charity partners.[1] The fixture was first played in the 1908–09 season, replacing the Sheriff of London Charity Shield.

    I wonder kama Urusi au France wana kitu inaitwa commuinity shield kufungua msimu.

    Mechi iwepo, lakini tutafute jina ambalo linawakilisha jamii yetu au historia pse .

    ReplyDelete
  2. Hapo Tff Angalau mmeonyesha busra kidogo sio kama kawaida yenu. sasa hao tunawataka wakiwa wameshashiba. tutawafunga bila kuwa na hofu hata kidogo. maana tukiwafunga wakiwa na njaa watalalama. maana hawakosi sababu wakishafungwa. tumewafunga wakadai Banka alikuwa chini ya kiwango, kumbe kiuongo wa Yanga alikuwa na uwezo zaidi. sasa mko kamili ndio tunawataka tena. Yanga Hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  3. Nikirudi kutoka kwenye maoni ya mdau wa kwanza hapo juu,sidhani kama kuna tatizo kukopi vitu vizuri katika kuleta maendeleo.yeye mwenyewe ametoa maoni kwa lugha ya kigeni hapo juu,je huo sio ulimbukeni na kukopi?leo china lnaitwa taifa kubwa na kuwa mbele kiteknolojia,yote yameanza kwa kukopi kutoka ulaya na america baadhi ya mambo.mdau soma historia ya maendeleo,kukopi vitu vizuri ndio mwanzo.Labda ungesema kuhusu mgao wa mapato Tff wapeleke kwa watu wenye shida hapo nyumbani

    ReplyDelete
  4. MBWEGELEMBWELEAugust 13, 2011

    @Utikae

    Kwa jinsi ulivyoelewa wewe, mada ilikuwa kucopy uwepo wa mechi ya ufunguzi au kucopy jina la mechi yenyewe ??????

    Back to the point,There is FA CUP in england,King`s Cup in spain,coppa Italia in Italy, DFB-pokal in Germany,etc

    Genius Utikae,Unaona uvivu wa aina gani kufikiria jina ambalo litawakilisha utamaduni au historia yetu .

    Kila jamii ina culture yake na identity. OK, mshindi wa 'FA CUP' ya tanzania alikuwa nani, na alikabidhiwa kombe na Malkia/Mfalme yupi msimu uliopita?

    JE,unajua kuwa kuna only one FA? ...na Tanzania tuna Footbal Federation ,sio Footbal association ????

    ReplyDelete
  5. Nakubaliana na Bro. hapa . Premier league ni ya uingereza, la liga ni ya spain, Bubesliga in Germany. Ligi Kuu ni ya Tanzania, hii mechi ya ngao inaweza ikatafutiwa jina , sio lazima iitwe community shield .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...