Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Richard Uku (katikati) akiwaeleza waandishi wa habari juu ya mkutano wa Benki ya Maendeleo wa Afrika (ADB) unaotarajia kufanyika mjini Arusha hapo mwakani. Wengine katika picha ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Said Magonya (kulia) na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma (kushoto).Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es salaam

Na Salama Juma-MAELEZO-Dar es salaam.

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ambao utafanyika mjini Arusha hapo mwakani.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha ADB, Richard Uku wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kuwahamasisha kufahamisha jamii juu ya mkutano huo muhimu.

Alisema kuwa hivi sasa timu kutoka ADB kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania imeshanza kuangalia maeneo ambayo mkutano utakapofanyikia ikiwa ni pamoja kuangali vyumba vya mkutano na huduma mbalimbali mjini hapo.

UKu aliongeza kuwa mkutano huo utakaofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Mwezi mei mwkani ni mwendelezo wa mikutano mbalimbali ambayo ufanyika kila mwaka kwa lengo la kujadili njia za kupunguza umaskini na kuboresha maisha ya wananchi.

Mkuu huyo alisema kuwa ADB imekuwa ikisaidia katika kutoa mikopo ya kusaidia ujenzi wa miundombinu na miradi mbalimbali ya maendeleo .

Kwa upande wake Kamishna wa fedha za Nje wa Wizara ya Fedha Said Magonya alisema kuwa ADB imekuwa msaada mkubwa kwa Tanzania na nchi mbalimbali za kiafrika katika kutoa mikopo nafuu.

Alitaja baadhi ya miradi inayofadhiliwa na ADB ni pamoja na ujenzi wa mradi wa umeme kutoka iringa, Shinyanga na ujenzi wa barabara ya Namanga ambayo inasaidia kuunganmisha Tanzania na nchi jirani.

Mkutano wa ADB mwaka huu ulifanyika mjini Lisbon , Ureno .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...