Asalaam aleykum, Ramadhan Maqbul
Ningependa kuwafahamisha kuwa Google ambayo inamiliki youtube kwa kushirikiana na wizara ya Habari na Utamaduni ya Saudi Arabia kuonyesha Ibada zote live toka Makkah. Hii ni mara ya kwanza kwa ushirikiano huo na hii inawapa nafasi waislam na wasio waislam wakifanya ibada katika msikiti mkuu wa Makkah.
Kwa wasio jua ni kuwa hiyo nyumba ambayo waumini wanazunguka inaitwa Kaaba na ilijengwa na nabii Ibrahim (Abraham) na mwanae Ismael (Eshmael) na wanaibada wanatakiwa kuizunguka mara saba huku wakimwomba Mwenyezi Mungu kama tulivyoamrishwa.
Tazama ibada live hapa:
Pia ningependa kuwapa link ya watu wanaotaka kusikiliza Qur'an online toka kwa wasomaji mbali mbali kama akina Abdelbasitm Shurain na wengineo...unaweza kusiliza hapa:
Mwisho naomba tuendeleze ibada zaidi katika hili kumi la mwisho na pia msisahau kutoa Zakatul Fitri mapema kwa wasio jiweza na hasa yatima na wengineo
wako katika uislam
Muyaka wa Kisarawe
Shukran sana mdau
ReplyDeleteNaomba michuzi uiache hii juu kwenye siku mbili tatu zilizobaki ili na wengine wapate fungu lao kwa kusoma na kusikiliza
Jazaak lwah,mungu akuzidishie brother kwa kutupa habari njema kama hizi.
ReplyDeleteRAJABU.
Manshallah
ReplyDeleteI have spent long periods just watching the live stream and listening to quraan
Allah yebarik