Meneja mawasiliano na mahusiano wa kampuni ya TBL, Bi. Editha Mushi akizungumzia msaada wa kiasi cha shilingi milioni 10 ambao TBL imetoa kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya sukari mjini Moshi.Kulia kwake ni Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi,Bw. Jafary Michael,Kulia ni mkurugenzi wa manispaa hiyo Bi. Bernedete Kinabo na mwisho ni meneja mauzo na usambazaji wa TBL kanda ya kaskazini Mashariki, Bw. Kasivo Msangi.
Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi, Bi. Bernadete Kinabo akipokea mfano wa hundi ya kiasi cha shilingi milioni 10 kutoka kwa meneja mauzo na usambazaji wa TBL kanda ya kaskazini Mashariki, Bw. Kasivo Msangi kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya sukari.
Mstahiki meya wa manispaa ya Moshi, Jafary Michael akimshukuru meneja mauzo na usambazaji wa TBL kanda ya kaskazini Mashariki, Bw. Kasivo Msangi kwa msaada wa shilingi milioni 10 zilizotolewa na TBL kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya sukari. katikati ni mkurugenzi wa manispaa hiyo.Bernedete Kinabo.
Afisa utawala wa kiwanda cha sukari cha TPC, Jafary Ally akiteta jambo na mkurugenzi wa manispaa ya Moshi,Bi. Bernedete Kinabo na Meneja mawasiliano mahusiano wa TBL,Bi. Editha Mushi kando ya barabara ya sukari inayojengwa kwa mchango kutoka TBL.
Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Bi Berdete Kinabo akionyesha barabara ya sukari ambayo tayari imeanza kukarabatiwa,nyuma yake ni Meneja mawasiliano mahusiano wa kampuni ya TBL Bi Editha Mushi,TBL imetoa kiasi cha shilingi milioni 10 kusaidia ukarabati huo.

Na Dixon Busagaga,Moshi

KAMPUNI ya bia Tanzania(TBL) imetoa msaada wa shs. Mil. 10 kwa halmashauri ya manispaa ya Moshi kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa barabara ya sukari yenye urefu wa Km. 2.6 kabla ya kujengwa kwa kiwango cha lami hapo baadaye.

Meneja mawasiliano mahusiano wa kampuni hiyo Bi Editha Mushi amesema fedha hizo ni sehemu ya mapato ya kampuni katika kuchangia na kutatua mahitaji ya jamii kama njia moja wapo ya kudumisha uhusiano
uliojengeka kwa miaka mingi.

Amesema ujenzi wa barabara hiyo hautasaidia tu kituo cha mauzo cha TBL lakini pia wananchi wa Moshi na maeneo mengine mkoani humo watapata fursa ya kufungua biashara mbalimbali katika maeneo hayo kwa kutumia mawasiliano ya barabara hiyo.

Akipokea msaada huo kutoka kwa meneja mauzo na usambazaji wa TBL kanda ya kaskazini Mashariki, Bw Kasivo Msangi, Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Bi Bernadete Kinabo amesema barabara hiyo ni muhimu kwa uchumi wa manispaa na makampuni yanayohudumiwa an barabara hiyo.

Amesema barabara hiyo ilishajadiliwa katika vikao vya bodi ya barabara mkoani ambapo zilikuwa zikihitajika zaidia ya shs. Bil. 3 katika kuijenga katika kiwango cha lami jambo lililoilazimu manispaa kuomba misaada katika taasisi na kampuni tofauti hususan yanayohudumiwa na barabara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. BIG UP TBL. KULA MBILI ANGANI ZA CHADEMA. NAONA MMEANZA KUUCHANGAMSHA MJI WA MOSHI KWA MAANA YA HUDUMA YA KINYWAJI CHETU CHA ASILI, AJIRA (DIRECT AND INDIRECT) NA MAPATO (KODI) NA PUNDE TU UCHUMI WA MOSHI UTAPAA. BI KINABO UMETUAMBIA ZINAHITAJI 3B HADI SASA ZIKO AU ZIMESHAPATIKANA NGAPI? LETE BAKULI NA HUKU BONGO TUKUCHANGIE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...