Mwanafunzi Zuhura Michenje (kushoto) wa Shule ya Sekondari Ilulu, mkoani Lindi, akifanya majaribio kwa vitendo baada ya shule hiyo kupata msaada wa vifaa vya maabara vyenye thamani ya sh. Milioni 11 kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika hafla iliyofanyika juzi shuleni hapo. Kutoka kulia ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu, Mkurugenzi wa Uhusiano wa kampuni hiyo, Steve Kilindo na Mkuu wa Mkoa huo, Said Sadick.
Wanafunzi wa Kidato cha Pili wa Shule ya Sekondari ya Ilulu, mkoani Lindi, wakiwa darasani kabla ya hafla ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya maabara na kampuni ya Bia Tanzania (TBL), shuleni hapo juzi. Vifaa hivyo vina thamani ya sh. milioni 11.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...