Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Ndanda,Wilayani Masasi wakichota maji kwenye mto uliopo katika kijiji hicho kwa ajili ya matumizi mbali mbali ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kupikia.mji huu ambao hali ya upatikanaji maji imekuwa ni ya shida sana hasa ifikapo kipindi hiki cha ukame kama wasemavyo wenyewe wakazi wa mji huu.
 Mama na Mwanae wakijiandaa kuondoka katika eneo la mto huo mara baada ya kufua na kusafisha mahindi  tayari kwa kuyaandaa kwa chakula.
 Watoto wakitoka kuteka maji katika mto huo na kuelekea majumbani kwao.
Kijana huyu akijiandaa kuelekea kuteka maji mtoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Serikali ya Kikwete itawaletea vitambulisho vya taifa msiwe na wasi wasi. Sasas watu kama hawa hawana maji safi lakini watakuwa na vitambulisho. Where is our priorities? they can't survive without water but they can live without National ID.

    ReplyDelete
  2. Milioni 50 kila idara zilikusanywa na wale jamaa wa wizara ya nishati na madini kwa kulipia kupitishwa bajeti ya ujanja-janja,haya sasa watu wanateseka hali hii.
    Hivi kweli bungeni wanapata picha kama hizi?Lakini naona ndio kujisahau baada ya kupigiwa kura au kuchaguliwa kuwa kiongozi.
    Inatia hasira sana kuona wananchi wanateseka na viongozi wakisukumwa wakiwa ndani ya magari yao.
    Wananchi hawana maji,mafuta,umeme,madawati,nk lakini viongozi wanapewa magari bure,dereva bure,chakula bure,mafuta bure,elimu bure,umeme bure nk na bado wanajiuzia mali za umma kwa bei chee,wanauza maliasili kwa faida zao na wanawaacha walipa kodi taabani kiasi hiki.
    Mungu atahukumu tu,ipo siku, kama sio wewe basi hata kizazi chako.

    ReplyDelete
  3. Nafikiri aliyepiga picha hizo amefikisha ujumbe vizuri lakini angalizo ni kuwa hapo ni kijiji cha Nangoo. Ndanda kama ndanda haina shida ya maji Nangoo ndio kuna matatizo hayo na huo mto uko Nangoo nafikiri muwe mnatoa taarifa zenu vizuri Ndanda kuna maji mengi na vyanzo vingi ya kutosha tunawashukuru lakini muwe mnafanya uchunguzi kabla ya kutuma ujumbe wenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...