Mafundi wakisambaza nyaya za mkongo wa Taifa ambao kwa sasa unasambaa kila mahali nchini na kuisogeza Tanzania karibu kabisa na njia kuu ya mawasiliano ya kasi duniani. Mpango mkubwa wa awali wa mkongo huo ulikuwa ni kusogezwa hadi mipakani ili nchi jirani ziweze kununua huduma hii kutoka kwetu, jambo ambalo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani juzi tu tayari Rwanda wameweka nia ya kuunganishwsa haraka iwezekanavyo. Nchi zingine zinazotegemewa kujiunga na mkongo wetu ni pamoja na Malawi, Zambia, Congo na Burundi. Hivi tunavyoongea wilaya takriban 17 nchini zimeshaunganishwa na mkongo wa Taifa na kazi inaendelea kwa kasi ili ufike katika kila wilaya ifikapo mwishoni mwa 2012.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ahsante mtoa hoja, ila sina hakika sana kuhusu Rwanda kama bado wanategemea kuunganishwa kutoka hapa kwetu. Habari ambazo nilizisikia ni kwamba wao waliishapata toka sehemu nyingine kwani sisi tulisua sua,,,

    ReplyDelete
  2. BASI SASA HUDUMA ZA INTERNET NA MAWASILIANO ZISHUKE BASI MAANA BADO NI EXPENSIVE SANA KULINGANISHA NA NCHI NYINGINE NA SPEED IONGEZEKE VILE VILE.

    ReplyDelete
  3. Safi sana ila wasiwasi wangu huo mfuniko wa manhole, Jamaa wa chuma chakavu wanapumulia pembeni tu

    ReplyDelete
  4. kweli kabisa. mimi nimeshakaa rwanda kwa mda kidogo. na kule wanatumie connection ya kenya ambao wao waliweka fibre kabla hata seacome hawajamaliza project yao. kuna project hap amjini ambayo ipo chini ya Simba net kwaajili ya cable internet na cable TV. isijekuchanganywa na huo mkongo wa Taifa i think ni vitu vilwili Tofauti kabisa.

    ReplyDelete
  5. Jamani Jakaya amefanya mambo mengi sana mazuri,CHUO,HIYO FIBRE,WAWEKEZAJI WA NGUVU WAKO MBIONI,KILIMO KWANZA,PROJECT YA MABASI KASI DAR,KINGAMBONI PROJECT-VIWANJA,UHURU WA HABARI,NA MENGINE MENGI AMBAYO YATALETA MATUMAINI ZAIDI.Ila inasikitisha jinsi yanavyofunikwa na mafisadi na kutochukua hatua kama angeact kwa hayo mambo wangeweza kuwin wananchi.inasikitisha sana.kwa swala hili litatupeleka mbali kimaendeleo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...