Salaam Aleykum ankal!
Naomba waislam wenzangu tumuombe mwenyezi mungu aweze kutujaalia tuupate usiku wa Laylatul Qadr!
Tujikumbushe namna ya kuupata usiku huu kwa kusoma maelezo yake yanayofuatia hapo chini!

Laylatul-Qadr- Vipi Uweze Kuupata Usiku Huu?
·         Nasiha Za Minasaba Mbalimbali
Tunaingia   kumi la mwisho, kumi ambalo ndani yake kuna siku tukufu, siku ya Laylatul-Qadr, ambayo ibada yake ni bora kuliko ibada ya miezi elfu.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):  ﴿ بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾
(( إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ)) (( وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ)) (( لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ))  ((تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ)) (( سَلَامٌ هِيَ حَتَّى مَطْلَعِ الْفَجْرِ))
BismiLlaahir Rahmaanir Rahiym
((Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatul Qadr,  (Usiku wa Makadirio[Majaaliwa]). Na nini kitachokujuulisha nini Laylatul Qadr?)) ((Laylatul-Qadr ni bora kuliko miezi elfu)) ((Huteremka Malaika na Roho (Jibriyl) katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo)) ((Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri))  [Al-Qadr: 1-5]
 Vile vile dalili katika Hadiyth mbali mbali zimethibiti kuhusu Fadhila za usiku huu mtukufu, na jinsi Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa hali yake katika siku hizi kumi za mwisho za Ramadhaan.
Baada ya kuzijua fadhila zake usiku huu mtukufu inakupasa Muislamu ujikaze katika siku kumi hizi za mwisho kuacha mambo yote yanayokushughulisha ya dunia na utumbukie katika ibada tu ili uweze kuupata usiku huo mtukufu, yaani ukukute wewe ukiwa katika ibada ili zihesabiwe ibada zako kama kwamba umefanya ibada ya miezi elfu.
Tukifanya hesabu miezi elfu hiyo ni sawa na umri wa miaka 83!  
1000 ÷ 12 = 83.3 yaani miaka themanini na tatu na miezi mitatu takriban.
Hivyo ikiwa Laylatul-Qadr imekukuta katika ibada ya aina yoyote, ikiwa ni Swalah (Qiyaamul-Layl), kusoma Qur-aan, kufanya aina za dhikr, kutoa sadaka, kulisha chakula, kuwasiliana na jamaa, kujielimisha au kuelimisha, kufanya wema kwa watu, yote hayo utaandikiwa kama umefanya hayo kwa umri wa miaka 83! Na juu ya hivyo ibada hiyo ya usiku mmoja tu ni bora zaidi kuliko ibada utakayoweza kufanya miaka 83 na miezi mitatu. Subhaana Allaah!
Jihadhari ndugu Muislamu usije ukakukuta usiku huu mtukufu ukiwa katika maasi au katika sehemu ukiwa  umeghafilika na ya dunia kama sokoni, magenge ya soga au michezo ya kupoteza wakati au kwenye televisheni ukiangalia misalsalaat, mipira na sinema zikakupita kheri zote za usiku huu. Utaona siku hizi Waislamu wengi wanashughulika kwenda madukani kutafuta nguo za 'Iyd khaswa kina dada wakiacha masiku haya yawapite wakiwa humo badala ya kuwa majumbani mwao au misikitini kufanya ibada na kutegemea kuupata usiku huu.   
Ni siku chache tu ndugu Waislamu ambazo zinakimbia kama upepo. Je, nani basi katika sisi atakayepuuza asiupate usiku huo? Na Nani katika sisi atafanya hima kuupata usiku huo? Kwani hatujui kama tutakuweko duniani mwakani kuzipata siku hizi au hata hatujui kama tutaikamilisha Ramadhaan hii. Basi tujitahidi kwa kukesha  siku kumi hizi na kuamsha familia zetu ili iwe kheri yetu kukutana na usiku huo mtukufu tuweze kupata fadhila zake hizo ambazo ni sawa na kulipwa malipo ya umri mrefu kama tulivyoona hapo nyuma hata kama hatutoruzukiwa umri huo.
 AMwenye Kuukosa Usiku Huu Amekula Khasara Kubwa
Hakika mwenye kuukosa usiku huo atakuwa amenyimwa kheri zake na itakuwa ni khasara kuukosa usiku huu mtukufu kama anavyosema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):   
عَنْ أَبِي هُرَيْرَة رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : لَمَّا حَضَرَ رَمَضَان قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  (( قَدْ جَاءَكُمْ شَهْرُ رَمَضَان شَهْرٌ مُبَارَكٌ اِفْتَرَضَ اللَّهُ عَلَيْكُمْ صِيَامَهُ تُفْتَح فِيهِ أَبْوَاب الْجَنَّة وَتُغْلَق فِيهِ أَبْوَابُ الْجَحِيم وَتُغَلُّ فِيهِ الشَّيَاطِين فِيهِ لَيْلَة خَيْرٌ مِنْ أَلْف شَهْر مَنْ حَرُمَ خَيْرهَا فَقَدْ حُرِمَ)) وَرَوَاهُ النَّسَائِيّ
Kutoka kwa Abu Huraryah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba ilipofika Ramadhaan, amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Umekujieni mwezi wa Ramadhaan, ni mwezi wa Baraka. Imefanywa Swawm kwenu kuwa ni Fardh, milango ya Pepo hufunguliwa na milango ya moto hufungwa na mashaytwaan hufungwa. Umo katika mwezi huu usiku ulio bora kuliko miezi elfu.  Atakayenyimwa kheri zake hakika kanyimwa haswa)) [An-Nasaaiy]

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hii blog sasa naona imeingiliwa na kirusi duh! asa tusiokua waislam hata hatuelewi hii naona mdau angeipeleka msikitini kwa wahusika ili awakumbushie huko

    ReplyDelete
  2. Alhamdulilhah!!! thanx a lot bro/sister

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza, kwani wanapoleta habari za kanisa huwa wasiokuwa wainjili wanashauri upeleke kanisani? Jaribu kuwa mstaarabu soma kinachokuhusu kama habari haikulengi kaa kimya.

    ReplyDelete
  4. WEWE BWEGE SANA ANONYMOUS WA KWANZA HAPO JUU.KUMBUKA HII NI BLOG YA JAMII NDIO MAANA KUNA HABARI MBALI MBALI ZINAWEKWA.SO KUWA MAKINI NA MSEMO WAKO.
    MDAU TOKA KULE KULE.

    ReplyDelete
  5. wewe mdau hapo juu hii blog mtu yeyeote anaweza kuposti kitu kwa hiyo acha maneno yako ya chuki na ubaguzi hii siyo blog ya kikristo peke yake,kama wewe haikuhusu sisi pia inatuhusu

    ReplyDelete
  6. wewe anonymous wa mwanzo hapo juu (wed aug 24, at 9.42 am 2011) wacha hizo kama kweli wewe mtanzania wacha hizo,kumbuka mwenye blog hii ni muislamu lakini mbona anaweka mambo yenu ya kikiristo mara nyingi sana na wala sisi hatu complain kama unalivyofanya hapo juu, wacha hizo wewe,kuwa mstaarabu kwani umelazimishwa usome au uingia katika hii blog.nahisi kirusi kimekuingia wewe tena inabidi ukamtafute mganga akupunge na kukupepea upoa roho yako.
    uncle michuzi post maoni yangu haya please

    na shukran sana sis/bro kwa kupost issue hii ya laylatu kadri nitamuombea huyu jamaa mungu amhidi amin.

    ReplyDelete
  7. Anonymous 1 acha udini wewe sio kila post iwe relevant kwako kuna mamilioni ya watu inawahusu.kama kwako sio sawa soma kitu ingine iruke hiyo.hii blog ni ya wote.hata wewe weka mambo ya kikanisa wapo watu watakushukuru.usikarahishs wenzio

    ReplyDelete
  8. Mdau wa kwanza hapo juu anzisha blogu yako ya kibaguzi,michuzi hana ubaguzi ndio maana utakuta anatuwekea hata taarifa za ibada za misa humu huku wasiokua wakristo hata hawalopoki kama ufanyavyo....maneno yako machafu hayatobadilisha chochote. Safari hii mtaumia sana tu. Magid pia anatuwekea makala zetu kama kawaida.

    ReplyDelete
  9. we anony "Wed Aug 24, 09:42am 2011" hapo juu naona umesahau kwamba hii ni Blog ya jamii sasa kama hukufurahishwa na ujumbe uliotolewa sio lazima usome kila habari inayotolewa humu. Kuna matangazo ya dini ya upande wa pili (naona ndo yako) yanatolewa humu wala ankali habanii na wala hatupigi kelele, na pia kwa kua hayatuhusu hua atusomi tona "scroll down" tunanatafuta habari zinazo tupendeza. Ushauri wangu ni kua jaribu kuwa mstarabu kidogo.

    ReplyDelete
  10. we anonymous wa AUG 24,42:00 acha ujinga kwani blog hii unasoma peke yako,ndo mana ikaitwa blog ya jamii,sasa kama ww unaona jambo halikuhusu ulianzaje kusoma si ungeendelea na khabari nyingine zilizowekwa.humu zinawekwa habari mbalimbali kama SIASA,BURUDANI,NA MAMBO MBALIMBALI YA KIJAMII.acha fitna we kama hujapata bahati ya kuwa MUISLAMU kausha tu acha wenzako wafaidike.KAKA MICHUZI ENDELEA KUTUPA FADHILA ZA MWEZI WA RAMADHANI achana na wasiopenda dini za wenzao.

    ReplyDelete
  11. wewe acha udini huko mwenye blog mwenyewe muislam....

    ReplyDelete
  12. MJINGA AKIISHIWA HOJA HUANZA KUKOSOA BILA SABABU,KAKA ANONYMUS ITABIDI UFUNGUE BLOG YAKO NA UTAFUTE WAKATOLIKI WENZAKO PEKEYENU MUWE MNA JITUMIA SMS,UONE KAMA KUNA MTU ATALAUMU,USISAHAU IANDIKE JINA JUU VATICAN,AU KANISANI AU HATA ROZARI HAKUNA ATAKAYE KULAUMU,COZ ALWAYS INTELLECTUAL HUWA ANAWEZA KWENDA NA WAKATI NA HUWA ANAUPUO WA KUSOMA ALAMA ZA NYAKATI,HIKI NI KIPINDI CHA CHA MFUNGO,JIFUNZE TOKA KWA WENZAKO WE HUONI HATA WAKRISTO WENGINE WANADIRIKI KUFUTURISHA SASA WEWE POST TU INAKUTOA ROHO,MMMHHHHH NADHANI UNAMAWAZOMGANDO,HATA MUSLIMS FOR SURE WANAHITAJI KUISHI NA DUNIA NDIO HII HII.SASA WE UNATAKA WAENDE WAPI.

    ReplyDelete
  13. Salaam Ankali! Shukurani kwa kuweka ujumbe wangu, mwenyezi mungu akujaalie kheri na baraka nawewe upate kuupata usiku huu! Waislam wenzangu mwenyezi mungu awarudhuku kwa kuutetetea ujumbe huu muhimu kwetu sisi!

    Mdau Dada Amina

    ReplyDelete
  14. We mchangiaji wa kwanza huna akili timamu!
    Heshimu imani ya mwenzako na usidhani ya kwako ni bora! Kwani wote ni viumbe kutoka kwa Mungu mmoja na sisi ni ndugu moja..kama huelewi wewe, wanaelewa wenzio!We mchangiaji wa kwanza huna akili timamu!
    Heshimu imani ya mwenzako na usidhani ya kwako ni bora! Kwani wote ni viumbe kutoka kwa Mungu mmoja na sisi ni ndugu moja..kama huelewi wewe, wanaelewa wenzio!
    Mkristu Mkatoliki!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...