Ofisa wa kitengo cha mawasiliano UNIC-Tanzania Usiah Nkhoma Ledama akiongea leo,jijini Dar.

Pichani kulia ni Muwakilishi wa Shirika la kazi-Tanzania (ILO),Bwa.Antony Rutabandibwa akifafanua zaidi kuhusiana na kitabu kinachoelezea kwa ufupi athari kubwa kwa Watoto zitokanazo na kazi za ndani, kwenye warsha ilioandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Tanzania ikiwakilisha mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,na kuwaalika waandishi wa habari na pia kuwafahamisha juu ya vipaumbele kumi vya programu hii na utekelezaji wake,Warsha hiyo imefanyika leo asubuhi katika hoteli ya Movenpick, jijini Dar es Salaam.Pichani kushoto ni muwakilishi wa UNESCO Henry Glorieu.
Ofisa wa kitengo cha mawasiliano UNIC-Tanzania Usiah Nkhoma Ledam akifafanua mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na Umoja wa Mataifa Tanzania kuanza kutekeleza program mpya ya miaka minne inayojulikana kama Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa - (UNDAP) 2011-2015, inayolenga kusaidia maendeleo ya Tanzania kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Pichani kati ni Muwakilishi kutoka UN-Tanzania,ambae alikuwa akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa habari kuhusiana na namna gani Umoja wa Mataifa Tanzania utaweza kuisaida Tanzania katika moja ya vipaumbele vyake kumi vya programu hiyo ya UNDAP kwenye kipengele cha Utawala Bora na utekelezaji wake,shoto kwake ni Dada Nora Pendaeli kutoka UN-Tanzania.

Pichani kulia ni Mratibu wa Shirika la Chakula Duniani-Tanzania (FAO),Dr.Vedasto Rutacholozibwa akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa habari kuhusiana na namna gani Umoja wa Mataifa Tanzania utaweza kuisaida Tanzania katika moja ya vipaumbele vyake kumi vya programu hiyo ya UNDAP katika kipengele cha Ukuaji wa uchumi na utekelezaji wake.

Mtaalamu wa masuala mbalimbali ya Watoto kutoka UNICEF-Tanzania,Dada Mona Aika akifafanua jambo kwa mmoja wa Waandishi wa habari aliyehudhuria warsha hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Movernpick jijini Dar leo.

Afisa Habari kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Tanzania (UN-Tanzania),Hoyce Temu akiwakaribisha wanahabari na wageni waalikwa katika Hoteli ya Moevenpick jijini Dar leo,kwenye Warsha iliyohusu Umoja wa Mataifa Tanzania kuanza kutekeleza program mpya ya miaka minne inayojulikana kama Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa - (UNDAP) 2011-2015, inayolenga kusaidia maendeleo ya Tanzania kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Baadhi ya Wanahabari pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria warsha hiyo.

Pichani ni Waratibu wa warsha hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...