Hongera uncle kwa kuendelea kuifanya blog ya jamii kuwa kimbilio la kweli kwa jamii.
Pamoja na nia nzuri ya serikali kuimarisha miundombinu ya barabara lakini naamini kuna baadhi ya wakandarasi tena wazawa hawana nia njema japo ni wepesi wa kulaumu kuwa wakandarasi wa kigeni waanakuwa wakipendelewa katika kupewa tenda za ujenzi wa barabara .

Leo napenda kutoa angalizo juu ya ubora wa ujenzi wa barabara ya Davis Cormer-Jet Club ya hapa Dar es   salaam ambayo pia inapita maeneo ya Dovya , Abiola , Buza , Sigara na Lumo. Ujenzi wa barabara hii ambao unaofanywa na kampuni inayoitwa NYANZA unatia shaka japo mimi si mtaalamu wa ujenzi wa barabara lakini najua miongoni mwa wapenzi wa blog yako ni wanataaluma katika fani tofauti ikiwemo ujenzi wa barabara .

Baadhi ya vitu vinavyonitia shaka ni aina ya vifusi vinayotumika kabla ya kumwagwa kwa lami na utandazwaji kwa kifusi .

Ubora vifusi vinayotumika vinanitia shaka kwani niliwahi kushudia layer ya kifusi ya chini kabisa ikiwa ni vifusi (mabaki) vya/ya nyumba zilizobomolewa kupisha ujenzi wa barabara hii ambayo hapo awali ilikuwa ya haina lami.

Isitoshe katika maeneo mengi mkandarasi ametandaanza kifusi hata katika vumbi lililokuwepo hapo awali . Mara nyingi nimekuwa nikishuhudia wakandarasi ambao kwa mtazamo wangu nawaona kama ni makini wakichimba kuondoa tabaka la juu la mchanga/udongo na vumbi kabla ya kuweka kifusi kipya , Kwa mkandarasi huyu naona kama anajaribu kubana matumizi sasa sijui kwa sababu gani au bajeti ya ujenzi wa barabara hii ilikuwa ndogo sana.

Japo amejaribu kupitisha barabara mpya juu ya ile ya kisusi ya mwanzo ambayo ilikuwa nyembamba , nilitarajia hata angefukua pembeni mwa barabara hii kuondoa udongo wa zamani na kujaza kifusi kipya ili kupata upana wa baaara bara atakayo . Hili halijfanyika na sina shaka litapunguza umri wa barabara hii.

Kwa angalizo hili natarajia wahusika wa ofisi/wizara ikiwemo moja ya mawaziri makini Mh John Pombe Magufuli watatupia macho ujenzi huu ambao naona ni moja ya ufisadi ambao watanzania wengi unatuumiza .

Wako
Mpenda Nchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kweli kabisa ndugu mdau...Shida ya wakandarasi wa namna hii hawana uchungu na nchi yetu. Hawaangalii ubora...hata km bajeti ni ndogo, sidhani km ni vema kuendelea na hatua ya ujenzi km fedha haitoshi. Hapo ujue kuna watu wanabana matumizi kwa faida yao binafsi. Mbona Waingereza hawapendi kuharibu reputation zao?? Km unaona bajeti haitoshi mkandarasi hakuna haja ya kuendelea na ujenzi, ni bora kukataa hadi fedha ya kutosha itolewe, kwa nini kulazimisha? Mimi sielewi hizi tenda huwa zinapitishwa vipi wakati wakandarasi hawana majina na uzoefu. Kwa nini ukubali kuiharibu nchi kwa tamaa?? Halafu TANROADS barabara hazirekebishwi zinapobomoka kwa nini? Kawaida Barabara zinahitaji matengenezo ya mara kwa mara kila zinapoharibika, nashangaa ninyi mmekaa tu. Wizara ya Ujenzi ni vema kufuatilia barabara zetu.

    ReplyDelete
  2. Barabara nyingi Tanzania zinajegwa kwa viwango vibovu sana,mfano mzuri ni ile barabara kubwa ya mbagala ni mbovu mno cjui ni kandarasi gani kajenga hiyo barabara, NA kwa mshangao hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kwa mhujumu huyu WA uchumi,haiwezekani barabara in less than 3 years umekuwa kama ilijejangwa 30 years ago,serikali imeliona hili?

    ReplyDelete
  3. Mtoa mada umesaidia sana maana nami nilikuwa nawaza hilo. Pia mimi sio engineer, ila kwa taratibu na mwenendo wa jamaa anayejenga hiyo barabara ni kweli inatia shaka, sijawaji kuona barabara inajengwa kwa kuweka mchanga ambao tayari umeoza, hii ni ya kwanza. Pili sijawahi kuona ujenzi wa barabara hauzingatii usalama wa maeneo husika mfano sehemu zenye majimaji kuwekwa mchanga ambao ni rahisi kubebwa na maji hili nalo limeliona Nyanza. Tatu, hajali hata watumiaji wa barabara, mfano tayari amefunga barabara yenyewe na kuruhusu njia za mitaani ambazo gari zake zenye uzito mkubwa zimeharibu na kufanya zisipitike hata na gari ndogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...