Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TAA) Suleiman S.Suleiman (kushoto miwani) pamona na Mhandisi Mwandamizi wa Kampuni ya SINOHYDRO CORPORATION LTD Tawi la Afika Mashariki Qin Chao wakitiliana saini mikataba ya ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Kigoma, katika sherehe iliyofanyika jijini Dar es salaam Sept,15,2011 ikiwa katika muendelezo wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara katika sekta ya Uchukuzi, Sherehe hiyo pia imehudhuriwa na Uongozi wa Wizara ya Uchukuzi,Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
Waziri wa Uchukuzi Omari Ndugu katikati akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa benki ya Dunia na wafanyakazi wa wizara hiyo.
Na Ismail Ngayonga-MAELEZO
BENKI Ya dunia (WB) imeipatia Serikali ya Tanzania mkopo wa Tsh Bilioni 95 kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vya ndege vya mikoa ya Bukoba, Kigoma na Tabora.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo leo Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini, Mhandisi Suleiman Suleiman alisema katika mkopo huo, Tanzania itachangia kiasi cha Tsh Bilioni 19.
Mhandisi Suleiman alisema mkopo wa ukarabati wa viwanja hivyo unakuja kufuatia upembuzi na usanifu wa kina uliofanywa na benki hiyo katika viwanja saba vya ndege katika mikoa ya Arusha, Bukoba, Kigoma,Tabora, Shinyanga, Sumbawanga na Mafia.
Kuhusu ukarabati huo, Mhandisi Suleiman alisema mchakato wa manunuzi tayari wamekwisha patikana na kunichosubiri kwa sasa ni kuanza kwa shughuli ya ukarabati huo.
Alisema kwa upande wa kiwanja cha ndege cha Bukoba ambao ukarabati wake unakuwa wa kipindi cha miezi 18 na kugharimu kiasi cha Tsh Bilioni 21, mkandarasi aliyeteuliwa ni Construzion Generali Gilardi S.p.A (CGG) kutoka nchini Italia wikishirikiana na kampuni ya Mwananchi Engineering and Contracting Company Limited MECCO ya Tanzania.
Akifafanua zaidi Suleima alisema viwanja vya kigoma na Tabora, mkandarasi aliyeteuliwa ni Kampuni ya Sinohydro Corporation kutoka nchini China na ukarabati wa viwanja hivyo unatarajia kugharinu kiasi cha Tsh. Bilioni 20 kwa upande wa Kigoma na Tsh. Bilioni 11 kwa upande wa kiwanja cha ndege cha mkoa wa Tabora.
Kwa mujibu wa Mhandisi huyo, Kwa upande wa muda mkandarasi wa kampuni ya Kichina amepewa kipindi cha miezi 18 kukamilisha ukarabati huo wa uwanja wa kigoma, wakati katika kiwanja cha ndege cha Tabora muda uliotolewa katika kukamilisha kazi hiyo ni kipindi cha miezi 15.
“Miradi ya ukarabati wa viwanja hivi vitatu utasimamiwa na kampuni ya SSI Engineers and Environmental Consultants ikishrikiana na Howard Humpresy (T) Limited ya Tanzania, NASUTO Associates ya Tanzania na Netherelands Airports Consultants B.V (NACO) ya Uholanzi kwa jumla ya kiasi cha Tsh Bilioni 3.9” alisema Mhandisi huyo.
Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Omari Ndugu aliishukuru Benki ya dunia kwa mkopo huo. kwani kitendo hicho kinadhihirisha dhamira ya benki hiyo ya kuimarisha na kuboresha sekta ya uchukuzi nchini.
Aidha Waziri Nundu aliitaka TAA kuhakikisha kuwa muda uliwekwa na wakandarasi hao wa kukamilisha ukarabati wa viwanja hivyo vya ndege unazingatiwa, kwani lengo la Serikali ni kuona kuwa viwanja hivyo vinakamilika kwa wakati uliopangwa.
Hizo pesa zitakakoishia kwishney...
ReplyDeleteAnkala umeona lebooooooooz, picha ya pili kutoka juu?
ReplyDeletematonya hawezi kubadilika hata akiwa ombaomba kwa miaka 100 nchi imeoza kila mtu anachukua chake wananchi wanateketea hata huduma ya usafiri kwa raia hakuna serikali imeoza inanuka rushwa na tamaa za mafisadi
ReplyDeletebig mistake nchi za kiafrika hautakiwi kuwapa pesa unatakiwa kuwapelekea mafundi wanakarabati and thats how mambo yatafanyika perfect otherwise hakitafanyika kitu viongozi wetu are so selfish all they think ni maslahi yao.
ReplyDeletemdau wa kwanza, umeona picha mbili za mwanzo? ya kwanza watu wana tabasamu la hali ya juu, kwani wanajua pesa za bure hizo za kumalizia project zao binafsi na kupeleka watoto ulaya.
ReplyDeletePicha ya pili watu wanahuzuni za hali ya juu wakijua kuwa pesa hizo ndio kwishney na hazitotumika kwa malengo wanayosikia hapa.
Ni ajabu picha mbili zilizopigwa sehemu moja kusherehekea jambo moja lakini sura kwenye picha zina ujumbe tafuati
Hizo pesa tunataka zitumike kuboresha viwanja vya ndege kama wafadhili walivyo dhamiria na sio ziishie kujenga VIP Terminal kwa ajili yenu tu maana tunawahamu nyie mlivyo wabinafsi
ReplyDelete