Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Umoja wa visiwa vya Comoro Dkt.Ikililou Dhoinine muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana(picha na Freddy Maro).
Tanzania na Comoro zimekubaliana kuharakisha mazungumzo na taratibu za kurahisisha na kulegeza masharti ya upatikanaji wa visa za usafiri kati ya nchi hizo mbili ili kurahisisha mawasiliano mbali mbali ukiwamo usafiri kati ya nchi hizo mbili.
Nchi hizo pia zimekubaliana kuharakisha majadiliano na taratibu za kufikia mwafaka kuhusu mpaka wa majini baina ya nchi hizo mbili pamoja na nchi jirani ya Mozambique.
Aidha, Comoro imeiomba Serikali ya Tanzania kuisaidia nchi hiyo kupata nishati ya mafuta ya petroli na dizeli ambayo Comoro inasema kuwa imekuwa ina uhaba mkubwa nchini humo kwa sasa.
KWA HABARI KAMILI,BOFYA HAPA
KWA HABARI KAMILI,BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...