Ankal wape wadau hii

Wadachi  wamewabwaga mabingwa wa dunia wa mpira wa miguu kwa kuwatoa katika nafasi ya kwanza waliyokuwa wakiishikiria.

Kwa mujibu wa ranking za soka zilizotolewa na FIFA tarehe 24 Agosti 2011 katika libeneke lake la www.fifa.com , inaonyesha Hispania inashika nafasi ya pili, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Ujerumani. 

Wababe wa soka dunia, Brazil imeporomoka toka nafasi nafasi ya nne iliyokuwa ikishika mpaka nafasi ya sita, ikipigwa kumbo na nchi za Uingereza (nafasi ya 4) na Uruguay (nafasi ya 5).

Nafasi
Nchi
1.
Netherlands
2.
Hispania
3.
Ujerumani
4.
Uingereza
5.
Uruguay
6.
Brazil
80.
Uganda
125
Tanzania

Katika orodha hiyo, Tanzania inaonekana kupanda kwa nafasi mbili toka nafasi ya 127 hadi nafasi ya 125, ikiziacha nyuma nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Kongo (nafasi ya 127), Kenya (nafasi ya 133), Rwanda ( nafasi ya 138), Ethopia (nafasi ya 140) , Burundi (nafasi ya 145), wakati kwa Afrika Mashariki nchi ya Uganda ndiyo inayoongoza kwa nafasi ya juu katika ranking hiyo ikiwa nafasi ya 80.

Mdau John.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mwanzo-.."wamewatoa katika nafasi ya kwanza waliokuwa wakishikiria"..Mara- "Brazil imeporomoka kutoka nafasi nafasi ya nne iliyokuwa ikishika mpaka nafasi ya sita"!..

    Mbona mawenge?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...