Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa hotuba na kuelezea uzoefu wa Tanzania kuhusu changamoto za sayansi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Sweden. Mhadhara huo uliambatana na safari ya Makamu wa Rais katika maabara mbalimbali zilizopo chuoni hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Uppsala Sweden, Bo Sundavist (katikati) na Mkurugenzi, Romain Murenzi, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ua Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo nchini Sweden. Mhadhara wa maadhimisho hayo ulifanyika jana nchini hapa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Prof. Mohamed Hassan (kushoto) Prof. Jean-Piere Ezin (wapili kushoto) na Prof. Mohamed Elton, baada ya kumalizika kwa Mhadhara wa kuhusu changamoto za sayansi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Sweden, jana.
 Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa Chuo cha Uppsala, Mikael Norrby, kuhusu Viumbe vilivyokaushwa na kuhifadhiwa katika Jumba la makumbusho la Gustavo Adolpho nchini Sweden, wakati Mama Asha alipotembelea katika Jumba hilo na kujionea mambo mbalimbali ya kisayansi yaliyomo katika Jumba hilo jana. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...