Mbunge wa Viti Maalum wa mkoa wa Mbeya,Dk.Mary Mwanjelwa akimkabidhi msaada wa magodoro,Mganga Mkuu wa jiji la Mbeya, Dk.Samuel Razalo, kwa ajili ya kusaidia wodi ya Wazazi iliyopo kituo cha Afya Ruanda-Mwanjelwa, mjini Mbeya.
Dk. Mwanjelwa anamkabidhi rasmi msaada wa magodoro 70,Mkuu wa kitengo cha Wazazi Meta, Dk.Peter Msafiri.
Dk.Mary akimjulia hali mmoja wa watoto aliyetajwa kwa jina la Siza Maige, ambaye alikuwa amebebwa na shangazi yake aitwaye Lucia Maige.Hapa ni chumba cha Wazazi hospitali ya Meta, mjini Mbeya.
MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Mbeya, Dk.Mary Mwanjelwa akimjulia hali Ofisa Muuguzi wa hospitali ya mkoa Mbeya, Edith Konga, aliyelazwa wodi namba mbili, kitengo cha Wazazi Meta.
MMOJA wa wana-CCM wa kata ya Ruanda, akiwa amejilaza katika moja ya magodoro yaliyotolewa msaada na mbunge Dk.Mary kwa kituo cha afya, Ruanda, kilichopo eneo la Mwanjelwa, mjini Mbeya.
MSAFARA wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya, kwa tiketi ya CCM, Dk.Mary Mwanjelwa, ukiwasili hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Wazazi Meta, ambapo Dk.Mary alitoa msaada wa magodoro 70 kwa ajili ya kusaidia wodi za kina mama na watoto.
mimi huwa sielewi hawa wabunge wanatoa hii misaada, kama yeye mbunge mzuri ni kukuhakisha kwamba tatizo nilitatuliwa na serikali na mpango wa kutatua tatizo unakuwa endelevu, sasa mbunge katoa msaada, je ataendelea kutoa msaada kwa vizazi vyote vinavyokujua, sijui kama huyu mbunge anafanya jambo hili kwa moyo mmoja au atafatufa umaarufu, naomba wananchi wenzagu tuwe tunachagua wabunge wenye upeo wa kutatua matatizo na kuleta maendeleo ya muda mrefu, tunajue kama hayo magodoro yamechukuliwa dukani kwa mtu halafu baadaye yanarudishwa, niwakilisha
ReplyDeleteShukrani kwa msaada Mary, lakini kwani lazima ujitangazeee, hivi hivi huo msaada haufiki au mwaka 2015 ndiyo umeanza!!!
ReplyDeletemaelezo ya picha ya kwanza na ya pili naona yamechanganywa .picha ya kwanza anaepokea msaada ni DR. MSAFIRI .MRS DAKAWA
ReplyDelete