Assallaam Alleykum Ankal Issah
Naomba nitolee hili dukuduku langu katika blog yako kama ikiwezekana!Nilikuwa naangalia katika blog yako leo nikaona ajali mbaya tena imetokea huko karibia na Chalinze watu kumi wamefariki tena,na hata haijapita hata wiki mbili tangia ajali ya Meli Zenj itokee!nimejaribu kuangalia katika Comments za watu nikaona mdau mmoja kaandika jambo la maana,na mimi ikanipelekea niandike hapo juu kwa kuwa sio watu wengi wanaangalia katika comments ndani ndani wanapitia tu hapa juu juu!
Mdau anashauri hivi!Ni bora ikaundwa wizara maalum ya kushughulikia maswala yote ya ajali.Nimeona huwo ni ushauri mzuri sana maana huyo waziri atafocus na vizibiti mwendo usalama wa katika Sea,Mito na Maziwa!Waziri atapanga watu wake katika hata barabara ili kuwaangalia madriver wanaoendesha magari kwa kasi na wanaoendesha usiku wa manane huku wakisinzia au wamekunywa pombe.au wengine wakitaka kufika mapema kwa ajiri ya trip nyingine au kuwahi maswala yao binafsi.
Hili swala la ajali kama huna mtu anae kuhusu ambaye alishapoteza maisha yake katika ajali pengine huwezi kuona umuhimu wa kufuatilia mambo ya ajali,,lakini kama kweli wewe ni mtanzania hata kama unaishi nje ya nje swala hili linakuhusu maana ukija nyumbani utatumia hizo hizo barabara na usafiri huwo huwo wa maji kama utapita tu angani lakini nduguzo tuko huku chini tunakwisha.na watu kugongwa kila siku.
Watu wengine huwa wanalalamika sana kwa mwendo mkali wa driver lakini wanashindwa kumwambia kwa kuwa driver wenyewe huwa hawajali maombi ya abiria ili mladi wameisha pokea hiyo nauli yao!
hiyo habari ya kusinzi nilishaishuhudia mwenyewe katika basi moja nilipanda kutokea huko mikoani,kwa kuwa mimi huwa ni mwoga sana watu wote walisinzia katika basi mimi nikamuomba mtu aliyekuwa kakaa karibu na driver ili akakae katika nafasi yangu nyuma mimi nikae hapo mbele karibia na driver.
Yaani Mungu si Athuman nilikuwa hata sijakaa nusu saa basi lilikuwa katika mwendo mkali mno,mbele kuna kona kali,,na hapo hapo kuna bonde refu mno,,,driver kasinzia mikono yake iko inalegea tu juu ya usukani!!
Yaani nilipiga makelele,ndo Driver kustuka gari limeisha toka barabarani ndo linataka kujitupa hukooo katika bonde refu,,yaani tungeisha wote katika basi,,Alhamudulillahi Tulipona na wote waliokuwa wamelala ndo wakaamka na wengine kuanza kulalamika kuwa walisha mwambia Drive apunguze mwendo na wengine wakasema hizi safari za usiku ni za kuibia tu zinakatazwa,watu walishangaa kuniona mbele karibia na driver wakasema kilichonipeleka hapo ni Mungu kutunusuru wote kuhusu usalama wa majini,,hasa tamaa ya kujali pesa badala ya uhai wa watu!
Mtu kama kiongozi unasimamia Meli kwa nini usikae mpaka mwisho kuhakikisha tiketi zilizokatwa ndo hicho kiasi cha watu wa kuingia ndani ya Meli?
watu wengi huwa wanakatia tiketi ndani ya Meli na hata train vile vile,kwa hiyo watu wanakuwa wengi kupita maelezo,,na mtu kama ukiwahi kukata tiketi masikini kumbe baadae wanaongeza watu na wewe huwezi kukuta imejaa na hali uko na tiketi ukaacha kusafiri,,yaani Meli inaanzia hapo bandalini maji yanaingia ndani kabla hata haijafika katikati ya safari kwa ujazo na uzito wa hali ya juu,basi masikini watu wanakufa wanajiona sasa ndio mwisho wetu hapa Duniani,,jamani kifo cha maji ni kibaya mno kila mtu anatapatapa ili kunusuru uhai yake!Fikilia watoto masikini!
Kama wenye mabasi ndio wanaawaajili madriver wasokuwa wazoefu basi ikitokea ajali compuni hiyo isimamishwe kwanza kwa usafiri ili iwe fundisho kwa mabasi mengine ya kwao kuangalia upwa madriver,,mimi katika maoni yangu naona kidogo driver mtu mzima ni muangalifu zaidi kuliko vijana.,
Na magari yanayopack barabarani usiku huwa yanasababisha ajali kwa sana niko mna binamu yangu alipata ajali kwa lori la mkaa kupaki njian tena mjini Dar tu karibu njia ya kwenda mbezi,Huku Ulaya Uarabuni wanavizibiti mwendo na kila kitu kimesimamiwa kwa ufasaha kabisa,,si watu kuingia katika nchi yao,wenye shida na ulinzi wa uhakika kila pembe hakuna wa kujifanyia mambo yake kwa mwenzake Sheria itamzibiti.
Mimi sidhani kama kuna kiongozi yeyote Nyumbani anaependa kuendelea kuongoza nchi yenye majanga ya ajali kama hizo za kwetu Tanzania,,jamani hii imekuwa too much!Kiongozi anaruka tu na ndege au usafiri wa usalama barabarani kisha anashuhudia wananchi wanateketea barabarani kwa kulamba lami,na kuywa maji ya bahari au ziwa,,Masikini watoto wadogo wamekufa hata Duniani walikuwa hajajajuwa chochote,,Mwenyezi Mungu awarehemu na awatulize katika Pepo yake Tukufu!
Viongozi wetu nahisi wana huruma wa kwenda kushuhudia wapi janga limetokea na kutoa mkono wa pole,lakini je mnashindwa nini,,kuzuia kabla ya hiyo ajali?Swaaaallii hilo jamani!!!
Hamuoni kama Mwenyezi Mungu anatukwepesha na majanga makubwa yasoepukika kama tsunami,,na mitetemeko ya Aridhi na njaa kama huko Somalia na vita vya wenyewe kwa wenyewe?
lakini hizo ajali ni utashi wetu unaosababishwa na uzembe wetu sisi wenyewe!Tunakushukuruni viongozi kwa kutoa mchango kwa ajali kama hiyo ya ?Zenj lakini Je! Bukoba mlitoa kama hiyo!!!ha ha ha au kwa kuwa iko pembeni mwa nchi na Zenj kisiwa kinachojulikana ulimwenguni au je katika hayo mabasi yanayopinduka kila siku je?mmeeenda kuvisit kwa hao wafiwa?,,,
Naona sasa ni sisi wananchi zam yetu tuingie Makanisani Misikitini tumuombe Mungu wetu kwa sana ili atupunguzie hizi Ajali na azidoe kabisa kwetu zisisikike hata ya Baiskeli!!!na tumuombe atuepushe na janga la Rushwa na ubinafsi yaani ufisadi,,na hivyo ndo vinachangia hayo maajali rushwa na uonevu ukizidi wasiri siri Mwenyezi Mungu anakushushieni ajali anakumbwa aliyefanya na asiyefanya kama Sodoma na Gomola.
Kwa leo ni hayo tu.
Wabillahi Tawfiq!
Hanifah MTz
Mimi sikubaliani kabisa na wewe ati iundwe sijui wizard ya kushughulikia ajali? Ndio mwanzobwa kuengeza serikali kuwa kubwa tu na ajali zitabaki palepale. Hii wizara iliyoko sasa hivi imeshindwa nini? Unashindwa kuwajibisha wafanyakazi unategemea hiyo wizara itafanya nini cha zaidi.
ReplyDeleteKwanza waukize idara inayohusika unajua au Ina inspect ni wafanya biashara wangapi kujua jinsi wanavyofanya maintenance ya magus, ndege au hizo vessels. 2 uliza ni Mara ngapi wanaangalia quality ya business drivers, na wanaoajiri watu wasioqualify wanalipa fine gani? 3 ajali ikitokea watu wana Iowa? Kama wanatakiwa kulipwa na hawajalipwa serikali inafanya nini kuhakikisha hao wafanyaBiashara wanafilisiwa? Leo basi linaanguka kesho linarudi na jina lingine.
Uongozi wote kuanzia juu mpaka chini unatakiwa kujibu maswali au watu wawajibishwe kikweli. Wako wTu wengi sana wanaweza kufanya kazi Kama hwawezui wao
Kaka Issa na dawati la blogu ya jamii,habari.
ReplyDeleteKwa leo sina mengi ila naomba nitoe mwongozo na angalizo kwa wadau wanaotoa mawazo yao kupitia blogu yetu hii.
Kumekuwa na matatizo mengi ya matumizi ya msamiati wa lugha ya Kiswahili kwa watumiaji.Dhana hii inajidhihirisha wazi pale watumiaji na watoa mawazo kwa njia ya maandishi wanaposhindwa kutenga dakika tano za kupitia na kuhakiki kazi zao wanazozinakilisha kwenye mtandao.Hali hii inapunguza au kuharibu kabisa dhima ya ujumbe uliokusudiwa kwani maneno mengi yanakosewa na kutufanya wasomaji kupoteza kiu na nia ya kuendelea kufuatilia kilichoandikwa hadi mwisho.
Mwongozo.
Kabla ya kunakilisha maandishi yetu kwenye mtandao,nashauri tuwe na utamaduni wa kupitia kazi zetu ili ziweze kuwa na sura ya utumizi sahihi wa msamiati wa lugha husika na zenye kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira.
Asante.
Tanzania viongozi ndo mnachangia yote haya,,mtatumaliza jamani,,,sijui mtamuongoza nani tenaaaaaa?Mungu Ibariki Tanzania na watu Wake!
ReplyDelete