Ndugu zangu,


LEO Jumatatu ya Septemba 19, 2011 ni siku ambayo blogu hii ilizaliwa miaka mitano iliyopita.
Ndio, ilikuwa ni siku ya Jumanne, Septemba 19, 2006. Ni siku hiyo ndipo kwa mara ya kwanza niliingiza picha ya kwanza kwenye mjengwablog na kuashiria uzinduzi wa blogu. Picha hiyo niliipiga eneo la Kinondoni Shamba.


Tangu siku ya kwanza, niliweka wazi kwenye fikra zangu, kuwa Mjengwablog iwe jukwaa litakalomtanguliza mtu wa kawaida. Iwe sauti ya ya wale ambao sauti zao hazisikiki. Ndio, nilidhamiria, na bado ni dhamira yangu, kuwa Mjengwablog iwe ni jukwaa la fikra huru.


Kuwa iwe ni mahali kwa watu kutoa mawazo yao bila kukwazwa na mitazamo tofauti ya kiitikadi. Miaka mitano imepita, nafurahia, kuwa bado naongozwa na dhamira hiyo.


Ni wengi waliochangia mafanikio yaliyopatikana hadi sasa. Nikiwataja kwa majina orodha itakuwa ndefu mno. Iko siku nitawatambua rasmi. Lakini, haitakuwa orodha ndefu nikiitaja familia yangu ambayo imekuwa mchango mkubwa sana kwangu; mke wangu mpendwa na ‘makamanda’ wangu wane ambao hutokea wakanikumbusha kwa kuniambia; “ Baba ona pale, inaweza kuwa picha nzuri kwa blogu!” Hakika, familia yangu imenitia moyo na nguvu katika mengi niyafanyayo ikiwamo ili la kublogu.


Na leo nina furaha kuizindua rasmi domain ya http://mjengwablog.com . Hivyo basi, Mjengwa. Blogspot. Com imetoka kwenye hatua ya blogspot na kuingia katika website ikitoa fursa nyingi zaidi nau salama zaidi kimtandao.


Ndugu zangu,
Ni imani yangu, kuwa kama mlivyokuwa mchango mkubwa tukaweza kwa pamoja kufikia hapa na kusheherekea miaka mitano ya kuanzishwa kwa blogu hii, basi, mtakuwa na mchango zaidi huko twendako.


Ahsanteni.


Maggid Mjengwa,
Msamvu, Morogoro.
Septemba 19, 2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...