Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu unaojumuisha wahandisi, Wabunifu majengo, Wakadiriaji na Makondrasi uliofanyika leo Mlimani City,jijini Dar es Salaam.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akimkabidhi Cheti Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dr. Ramadhani Dau (wa pili kulia) kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo kwa Makondrasi wazalendo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dr. John Magufuli.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dr. Ramadhani Dau (kulia) akiwa ni mwenye furaha mara baada ya kukabidhiwa Cheti na Rais Kikwete ikiwa ni kutambua mchango mkubwa wa Mfuko kwa Makondrasi wazalendo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dr. Ramadhani Dau pamoja na wadau wengine wakifatilia mkutano huo.

Picha ya Pamoja.
Na Alfred Ngotezi
Rais Jakaya Kikwete leo amemkabidhi Cheti Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo kwa Makondrasi hapa nchini.
Rais Kikwete, ambaye alikuwa mgeni kwenye ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu uliojumlisha wahandisi, Wabunifu majengo, Wakadiriaji na Makondrasi alitoa zawadi hiyo kwa niaba ya Bodi ya Wakondrasi.
Mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu, kutoka nje na ndani, ulianza tarehe 5 na utakwisha tarehe 7 Septemba mwaka huu. Baadhi ya wajumbe walitoka Afrika Kusini, Zambia, Kenya na Malawi.
Akiongea kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mjini Dar es Salaam, Rais aliimwagia sifa NSSF kwa juhudi zake za kuinua sekta ya makondrasi hapa nchini.
NSSF inajenga nyumba 300 za gharama nafuu kwa ajili ya wanachama wake na wananchiwengine huko Mtoni Kijichi jijini Dar es salaam. Mradi huo unafanywa na Makondrasi wazalendo ambao wamepewa kazi hiyo na NSSF.
Rais pia aliwapongeza wahandisi, Wabunifu Majengo, Wakadiriaji na Makondrasi walioandaa mkutano huo na kuwataka wajiunge pamoja ili waweze kupata uwezo mkubwa wa kufanya kazi.

Rais Dr. Jakaya Kikwete (kushoto) akimkabidhi cheti Mkandarasi bora wa kike wa kampuni ya IBRA Building Contructor and General Supplies LTD, Bi. Maida Waziri wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa Wahandisi na Wakandarasi nchini kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es- Salaam jana.katikati ni Waziri wa Barabara wa Kenya,Franklin BETT.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi Mkandarasi bora anaechangia michango ya huduma za jamii katika sekta ya ujenzi Bw, Dismas Masalu Dede wa kampuni ya ujenzi ya Dema.Contruction Co. Ltd.
Mkandarasi Bora Mwanamke nchini kutoka kampuni ya IIBRA Building Contractor and General Supplies LTD, Bi Maida Waziri akionyesha cheti chake baada ya kukabidhiwa na Rais Dr. Jakara Kikwete baada ya kufungua mkutano wa siku tatu wa Wahandisi na Wakandarasi katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akitambulishwa kwa Waziri wa Barabara wa Kenya Mh. Franklin Bett (kushoto) na Waziri wa Ujenzi, Dr. John Magufuli (kulia) alipowasili kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Makandarasi na Wahandisi kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya sekta ya Ujenzi.
Baadhi ya wanafunzi bora waliofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi wakiwa katika ufunguzi wa mkutano wa Wahandisi na Wakandarasi wa siku 3 uliofunguliwa na Rais Dr. Jakaya Kikwete jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
kikundi cha sanaa cha JKT kikitumbuiza katika mkutano.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...