Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mheshimiwa Zhai Jun akisaini kitabu cha wageni pindi alipofika kwenye ofisi za Ubalozi wetu nchini China kwa maombolezo ya wahanga wa ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander iliyotokea hivi karibuni huko Zanzibar, kilichofunguliwa na Ubalozi wa Tanzania, Beijing China.Kulia ni Balozi wetu nchini China,Mh. Balozi Omar Ramadhan Mapuri
Mheshimiwa Zhai Jun pia alisaini kitabu cha Maombolezo  cha Ubalozi  maombolezo ya wahanga wa ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander iliyotokea hivi karibuni huko Zanzibar.
Balozi wa Ghana nchini China, Mheshimiwa Bibi Helen Kofi alikuwa miongoni mwa mamia ya wageni waliojitokeza kusaini kitabu cha maombolezo.
Mheshimiwa Balozi Helen Kofi akipokea maelezo ya ajali kutoka kwa mwenyeji wake Mheshimiwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri baada ya kusaini kitabu cha maombolezo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...