IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR INATOA SHUKRANI NYINGI NA ZA DHATI KWAKO KWA MASHIRIKIANO ULIYOIPA WAKATI WA JANGA LA AJALI YA MELI YA MV. SPICE ISLANDERS ILIYOTOKEA HIVI KARIBUNI KATIKA MKONDO WA NUNGWI KISIWANI ZANZIBAR.

MASHIRIKIANO MLIYOIPA YAMEWEZESHA KUTOA TAARIFA MBALI MBALI ZA UHAKIKA NA KURIDHISHA KWA WANANCHI AMBAZO ZIMESABABISHA UTULIVU NA AMANI KATIKA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA WAKATI WOTE WA TATIZO HILO LILIPOKUWA LIKITAFUTIWA UFUMBUZI.

BILA MASHIRIKIANO YENU NA KUWAPASHA HABARI WANANCHI JUU YA TOKEO HILO TUNAAMINI KUWA HALI ISINGELIKUWA SHUWARI NA UTULIVU WAKATI WOTE SERIKALI ILIPOKUWA IKILISHUGHULIKIA TATIZO HILO.

TUNAKUSHUKURUNI TENA NA KUOMBA KUZIDISHA MASHIRIKIANO KATIKA MASUALA YOTE YANAYOHUSU HABARI HAPA NCHINI ILI KUFANIKISHA KAZI ZETU.

NATANGULIZA SHUKRANI ZA DHATI KWENU.

IMETOLEWA NA:

IDARA YA HABARI MAELEZO

ZANZIBAR

15/09/2011

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...