Wazungu wenyewe hawana tabu washakielewa kilichoandikwa wana furaha tele wakijiandaa kuingia. 
Hapo ndio mlango wa kuingia katika uwanja wa Ndege wa Kigoma ukisoma hayo maandishi utajua kinachoendelea ni nini!  
KAPINGAZ Blog inawaomba wahusika wa Uwanja huu warekebishe hayo maneno hapo wanajiaibisha na pia wanauaibisha uwanja huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Kweli kule ni mwisho reli!! Jamani hata kuandika tu kwenye tangazo lugha inakuwa shida?? Mh. Zito tunaomba utusaidie kuwakumbusha wapiga kura wako warekebishe tangazo hilo!! Linaitia aibu Kigoma!!

    ReplyDelete
  2. Duuuuuhhhhhhh, what the hell is this and who approved it???! Ukisikia songombingo ndio hii sasa, yaani hadi nasikia aibu endapo watu wa nje (non-Tanzanians) wataicheki hii ishu, duuuuuuuuuuuhhhhh!

    ReplyDelete
  3. Acheni kutumia lugha za watu kama amzijui. Mbona kiswahili chetu mswazo tu na wageni wanakifagilia? Ila ni aibu, karibu mwaka unaisha tangu tangazo ili litolewe kwa michuzi. Wahusika hawapo au ndio ufisadi hata wa kubadili maandishi? Itabidi tumuombe Michuzi afungue kituo cha redio pengine itasaidia. Shame on you wahusika!
    Mdau skandinavian

    ReplyDelete
  4. This is embarrassing and it shows the outcome of a poor education system. After seeing this, would you still board a flight from Kigoma or take your chances elsewhere?

    ReplyDelete
  5. Icho ni Kiinglish cha Kigoma, wala hakuna tatizo hapo, Ndio maana mpaka hawaoni kwa nini wabadilishe..lo!

    ReplyDelete
  6. kama michuzi unaweza wapata dc, pc na wabunge wa kigoma naomba uwaonyeshe haya matangazo. mimi nilifikiri ulipo post hii last time labda wahusika wangeliona na kurekebisha lakini inaonekana hawajaona. pengine hakuna mtu yeyote kutoka huko anatambua haya makosa.

    ReplyDelete
  7. Wakubwa si wanapitia VIP wataona saa ngapi hiyo international airport ya dar yenyewe vindumbwendumbwe ukipanga foleni ya immigration unasikia harufu choo kipo hapohapo umeona wapi. Bongo kweli tambarare kula uende.

    ReplyDelete
  8. Ukweli ni kwamba English sio lugha yetu. Hata hao wadhungu wanalijua hilo. Kwa hiyo simshangai aliyeandika hilo tangazo. Ninaye rafiki yangu mmarekani mweusi aliwahi kuniandikia barua enzi hizo za barua. Kwa kweli kdhungu chake kilikuwa kibovu sana na amezaliwa kule na kukulia kule. Mimi najua Kiingereza vizuri kabisa lakini niko proud sana na Kiswahili chetu. Siwezi nikaacha kuongea kiswahili pale ninapoona nakihitaji eti kwa vile wazungu wataniona sijui lugha yao. What a hell is English? Ni lugha tu ya mawasiliano.

    Cha msingi tu ni kwamba ujumbe umeshafika na tunatarajia wanaojua kiingereza vizuri wataliandika vizuri hilo tangazo.

    Lakiniwatanzania mliosoma hamtaki pia kwenda kufanya kazi kigoma. Matokeo yake ndio hayo. Wanaokotwa watu tu ili mradi wanaweza kubabaishababaisha.

    ReplyDelete
  9. MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE WATUELEZE HAPO KIGOMA KUNA MENEJA WA UWANJA ALIYEENDA SHULE AU UMEPIGWA UNDUGUNAIZESHENI? MAANA HATA MTOTO WA FORM TWO PENGINE ASINGEANDIKA HICHO KIGOMALISHI KATIKA SEHEMU MUHIMU KAMA HIYO. MKURUGENZI WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NAE NI TATIZO ASITUAMBIE HAJAWAHI KUONA HILO TANGAZO LILILOANDIKWA KWA KIGOMALISH.

    NA HAYO NDIO MATUNDA YA MIAKA HAMSINI YA UHURU...MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  10. Hayo maandishi yasibadilishwe na yabakie hivyo hivyo kama yalivyo. Hii ndiyo njia nzuri sana ya kuwakumbusha wazungu kama wao hapa ni wageni tuu na lugha yao hapa kwetu ni lugha ya kigeni.

    Jee, kwani sehemu ngapi zinabandikwa matangazo kwa lugha ya kiswahili na hakiandikwi kiswahili fasaha lakini hamsemi kitu? Tuondoleeni utumwa wenu wa kiakili hapa. Tena wajinga zaidi ni wale ambao eti "this is embarassing"... pambafu kabisa, it is only embarassing because you are living your life up to wazungu's expectations". Na hayo ndiyo matatizo ya "kusoma sana".

    ReplyDelete
  11. Ndio Tanzania hiyo. Hapo kuna meneja, naibu meneja, wasaidizi kibao na wote wanapata mishahara. Wabunge na viongozi wote wakuu wanatumia huduma hiyo hiyo. What a shame kwa wageni jamani! Na bado mnasema mnataka kudumisha utalii! Wake up people

    ReplyDelete
  12. Hi ni aibu kabisa nadhani hapo kuna meneja wa uwanja ina maana hata yeye yupo confortable na hayo maandishi kwanza yameandikwa kienyeji sana-Nina wasi wasi na elimu za watawala wa uwanja huo

    ReplyDelete
  13. hiyo ndio karumanzila usinitaraiiii bwana,,,,,,,,,.....

    ReplyDelete
  14. Narudi hapa hii picha ni ya zamani, nadhani hilo tangazo halipo tena pale, picha ya sasa inakuja

    ReplyDelete
  15. muda mwingine, ankal usiwe unapost vitu bila kuwa na uhakika navyo ili mradi tuu umepost,hayo maandishi yalishafutwa kitambo,acha kurudiarudia mambo ili mradi watu wacomment,yapo mazuri pia yanayofanywa na taasisi iyo mbona huyarudiirudii? lete mada mpya bwana walishasikia walishayafanyia kazi,mdau unaonekana hujapita kitambooo

    ReplyDelete
  16. Kigoma ni mji lakini Tabora nichibokoo

    ReplyDelete
  17. Jambo nipe senti moja, ee jambo jambo wekupakekoweko ohh jambo la, jambo nime senti moja, eeh jambo jambo.......

    ReplyDelete
  18. HII SI KWELI JAMANI MSIWE WAPUUZI WA KUAMINI KILA KITU. USANII UNAFANYIKA KUWAFURAHUSHA TU. MI NILIPITA HAPO JULY MWAKA JANA NA SIKUONA MAANDISHI HAYO, NA APRIL MWAKA HUU KWA KUWA NILISHASOMA HILI TANGAZO NIKAJIRIDHISHA TENA HAKUNA KITU KAMA HICHO

    ReplyDelete
  19. Kilicho nisikitisha kabisa sio lugha ila ni jinsi tangazo lilivyo hata wameshindwa kuleta fundi wakuwawekea bango zuri je hizo kodi za uwanja wa ndege huwa zinaenda wapi hapo ufisadi tu

    ReplyDelete
  20. Mimi sijui kizungu wala kigomalish na ndio maana sina changu. Hata hivyo Wengi mnalalama lugha ya English au kimombo iliyotumika ni mbovu kwa tangazo hilo na kujisifu oh! cc kiiglish twakijua na wengine kusema hata mtoto wa form two asingaliandika hiko kigomalish. Mbona sijaona watu kujenga ama kusaidia kuandika hiyo lugha sahihi ya kiinglish hapa ili wahusika na kama mimi tukajifunza? Au twapenda kulaumu tu bila kujenga. "Hakika mbora wenu ni yule aliye na elimu na akafundisha wasionayo".

    lebeneke la jamii oyee!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...