![]() |
Hayati Joycelyn Mkamsuri Archibald Marealle |
Mama yetu Joycelyn Mkamsuri Archibald Marealle leo hatuamini kama ni mwaka mmoja umepita tangu ulipotuacha siku ile ya alhamisi saa mbili na nusu asubuhi tarehe 2/9/2010. Mama siku ya leo inaleta kumbukumbu zisizoelezeka na zisizostahimilika.
Mama ni vigumu kukubali kuwa haupo nasi ila hatuna budi kumshukuru mungu kwani alikupenda zaidi. Mama umetuacha mapema tukiwa bado tunakuhitaji kwani wewe ulikuwa ndiyo nguzo na mhimili wa maisha yetu.
Unakumbukwa sana na watoto wako Emily na Leonard. Mkwe wako Carolyne, wajukuu zako Vanessa, joycelyn na Eva. Pia Kaka na dada zako pamoja na ndugu zako ukoo wa kina Sawaya Mawalla na ukoo wa Marealle. Marafiki zako wote, na majirani zako wa drive inn estate.
Tunamuomba mwenyezi mungu ailze
roho yako mahali pema peponi,
Amina.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...