Mwendesha pikipiki akipita pembeni ya daraja dogo linalojengwa kwenye sehemu ya barabara ya kutoka kiwanda cha vinywaji baridi cha pepsi kwenda nyamkazi itakayotengenezwa katika kiwango cha lami na manispaa ya Bukoba, barabara hiyo ilikuwa kero kubwa kwa wananchi, ilikuwa haipitiki wakati wa mvua.
sehemu ya daraja dogo linalotengenezwa na kampuni ya peter Mulima liliko kwenye sehemu ya barabara itakayofanyiwa matengenezo makubwa na manispaa ya Bukoba yenye urefu wa kilomita 2 toka eneo la kiwanda cha pepsi hadi nyamkazi.Picha/Habari na Audax Mutiganzi,Bukoba. 

MANISPAA ya Bukoba imeanza kuifanyia ukarabati mkubwa barabara iliyokuwa inaleta kero kubwa kwa wananchi hasa nyakati za mvua yenye urefu wa kilomita mbili toka eneo la kiwanda cha kusindika vinywaji cha pepsi hadi eneo la Nyamkazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Bukoba Khamis Kaputa kwa vyombo vya habari barabara hiyo itatengenezwa kwa kiwango cha lami na ikimalizika itaigharimu manispaa hiyo zaidi ya shilingi milioni 450.

Kaputa alisema barabara hiyo inafanyiwa ukarabati na kampuni ya ujenzi ya Mulima yenye makao makuu yake mkoani kagera,alisema kampuni hiyo tayari imeishaanza hatua zake za awali ukarabati wa barabara hiyo.

Alisema kwa sasa kampuni hiyo imeanza kutengeneza kalvati kubwa eneo la nyamkazi ambapo mkondo mkubwa wa maji ulikuwa ukikatiza kwa wakati wote hasa wakati wa mvua, aliongeza kwa kusema mkondo huo ulikuwa unaifanya barabara hiyo isipitike kwa urahisi.

Mkurugenzi huyo mtendaji alisema mbali na kuiwekea lami barabara hiyo kazi nyingine zitakazofanyika wakati wa zoezi la ukarabati wa barabara hiyo kuwa ni pamoja na upanuzi mdogo.

Kaputa alisema barabara hiyo ilikuwa ni kikwazo kwa wakazi wa manispaa waishio maeneo ya Nyamkazi, alisema manispaa ya imeamua kuifanyia ukarabati barabara hiyo ili iweze kupitika kwa wakati wote.

Aliendelea kusema kuwa kwa sasa wakati ukaranati unaendelea wakazi waishio eneo la Nyamkazi kwa sasa wametengenezewa barabara ya muda kwa kuwa barabara inayofanyiwa ukarabati imefungwa.

Alimaliza kwa kusema kuwa manispaa ya Bukoba ina mkakati mkubwa wa kuzitengeneza barabara za manispaa hiyo katika kiwango cha lami, alisema kwa sasa manispaa hiyo inaendelea kuikarabati barabara toka ujenzi hadi soko la Kashai na nyingine eneo la Nyakanyasi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...