Pambano la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) limeingiza sh.148,220,000. Mechi hiyo ilichezwa Septemba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,892. Viti vya kijani ambavyo kiingilio kilikuwa sh. 3,000 ndivyo vilivyovutia mashabiki wengi ambapo 17,650 ikiwa ni zaidi ya nusu ya mashabiki wote walinunua tiketi kwa ajili ya viti hivyo.

VIP A ambapo ndipo kulikokuwa na kiingilio cha juu cha sh. 30,000, jumla ya mashabiki 394 walinunua tiketi kwa ajili ya eneo hilo. Viti vya bluu ambapo kiingilio kilikuwa sh. 5,000, mashabiki walionunua tiketi walikuwa ni 8,166.

Viingilio vingine katika pambano hilo vilikuwa sh. 7,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 VIP C na sh. 20,000 VIP B.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ungetupatia na matumizi ingekuwa jambo jema ndugu Wambura

    ReplyDelete
  2. TFF baada ya Matokeo ya Juzi kati ya Afrika ya Kati na Morocco(O-0) kundi letu bado liko wazi kwa timu yoyote(Morocco,Afrika ya Kati,Tanzania,na Algeria).Mimi niko tofauti kidogo na watu wanaoilaumu timu yetu ya Taifa.Vijana wanajitahidi sana..kupata pointi 2 kwa Algeria siyo kazi ndogo.(Angalieni viwango vya FIFA jamani)Kundi letu ni gumu ndiyo maana makundi mengine yameshapata wawakilishi kabla ya mechi za mwisho sisi kundi letu linasubiri mechi za mwisho.Mpira wa miguu ni mchezo wa Maajabu,,Tanzania bado ina uwezo wa kuwa kinara wa kundi hilo kwa 'goal difference"!!Ni Mipango tu ya kuifunga Morocco kwao goli nyingi(kuna wanaosema haiwezekani..Inawezekana)

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...