Mwenyekiti wa Mbio za Mbuzi, Karen Stanley (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Septemba 24 mwaka huu. Kulia ni Meneja Chapa na Matangazo wa NBC, Arden Kitomari ambaye benki yao ni mmoja wa wadhamini wa mbio hizo.
Meneja Chapa na Matangazo wa NBC, Arden Kitomari (kulia)akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam kuhusu udhamini wa benki hiyo iliyotoa shs milioni 12 kudhamini mashindano ya mbio za mbuzi zinazotarajiwa kufanyika Septemba 24 mwaka huu. Kutoka kushoto ni Mwandaaji wa mbio hizo Vanessa Morgan na Mwenyekiti wa Kamati ya Mbio za Mbuzi, Karen Stanley.
Meneja wa Shirika la Ndege la Uingereza (BA) nchini, Saada Juma(kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wao katika mashindano ya mbio za mbuzi yanayozotarajiwa kufanyika Septemba 24 mwaka huu. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mbio za Mbuzi, Karen Stanley na Meneja Chapa na Matangazo wa NBC, Arden Kitomari ambaye benki yao imetoa shs milioni 12 kudhamini mashindano hayo.
Kweli jamani kweli?
ReplyDelete