NDEGE INAVYO ONEKANA BAADA YA KUPATA AJALI.
BAADHI YA WATU WALIO FIKA ENEO HILO LA TUKIO KUTOA MSAADA BAADA YA AJALI HIYO.
HIVI NDIVYO NDEGE ILIVYO UMIA BAADA YA KUANGUKA ENEO LA NANE NANE UYOLE MBEYA.
ABIRIA WA NDEGE WAKIWA NA FURAHA MALA BAADA YA KUPONA KATIKA AJALI HIYO ILIYO TOKEA LEO ASUBUHI MAENEO YA NANE NANE,UYOLE MKOANI MBEYA.

Ajali ya ndege namba 9J-BIO SESINA 206, imetokea leo asubuhi majira ya saa tatu eneo la Nanenane Uyole jijini Mbeya na abiria wanne wanusurika kifo na hakuna aliyefariki.

Abiria walionusurika kifo ni pamoja JVER WAAK Umri wa Miaka 49 ambayealikuwa Rubani, Raia wa Afrika Kusini, Bwana CHRISTIAN BASIL MMASI umri miaka 30, Ambaye ni Afisa Utawala wa mashamba ya Kapunga wilaya ya Mbarali, Balozi MOHAMMED RAMIA kabula leke ni Mmakua mwenye umri wa miaka 64, mkazi wa Masaki jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyakazi EXPORT TRADING na Bwana SUNNY TAYIR mwenye umri wa miaka 50 ambaye ni Mhindi na ni mfanyakazi wa EXPORT TRADING.

Na chanzo cha ajali hiyo Hakijafahamiaka mpaka sasa.

Imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Bwana ANACLET MALIMBISA.PICHA ZETU NA MBEYA YETU BLOG

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. hahahahaha hahahaha tumepona wangu mungu si asumani hahahaha mimi sipandi tena hivi vibajaji vinauwa sana hahahaha mafuta yaliisha hahahaha

    ReplyDelete
  2. Mbeya kunani?? flight-unfriendly??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...