Waziri wa Afya  na maendeleo ya Jamii wa  Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Mhe. Juma Duni Haji,  akihutubia Mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani  kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na changamoto zake.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeungana na mataifa mengine  duniani  katika  majadiliano ya kufatufa njia muafaka na zenye gharama nafuu  za  kuudhibiti na kutibu magonjwa yasiyo ambukizi.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete. Waziri wa Afya  na maendeleo ya jamii kutoka Serikali ya mapinduzi  Zanzibar, Mhe. Juma Duni Haji, amesema magonjwa yasiyo ambukizi yanaendelea kuwa mzigo mkubwa hususani kwa familia maskini.

Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa, wamekutana kwa siku(jumatatu na jumanne) mbili kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu magonjwa manne ambayo si ambukizi. Magonjwa  hayo ni Kansa, Kisukari, Ugonjwa wa Moyo na Ugonjwa wa  Mapafu.

“Gharama za kutibu magonjwa haya ni mkubwa mno. Karibu kila familia ambayo imeathirika na  moja ya magonjwa haya inatumia asilimia 40 ya kipato chao kugharamia matibabu.  Haya ni magonjwa yanayosababisha   familia nyingi kuwa maskini” akasema  Waziri Duni ambaye ni kati ya mawaziri watatu walioambatana na Mhe. Rais Kikwete kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 66 wa  Umoja wa Mataifa ambao unaanza siku ya jumatano.

Mkutano wa Kilele kuhusu magonjwa yasiyo ambukizi ni kati ya mikutano kadhaa ya kilele ambayo inafanyika kabla ya  Mkutano Mkuu.

Kutoka na gharama kubwa ya kutibu magonjwa hayo, Waziri Juma Duni amesema, Tanzania inasisitiza  umuhimu wa magonjwa hayo kuingizwa katika ajenda za  Kimataifa za Maendeleo.

Akasisita kuwa ongezeko la  magonjwa yasiyo ambukizi   kumesababisha    changamoto kubwa katika mfumo  uliopo wa utoaji wa huduma za afya.

Akizungumzia uzoefu wa Tanzania , Waziri amesema  serikali  ilizindua mwaka 2009 mkakati wa kitaifa kuhusu magonjwa yasiyo ambukizi. Mkakati huo unalenga  pamoja na mambo mengine kuhakikisha  upatikanaji wa huduma za afya pamoja na utudhibiti wa magonjwa hayo.

Aidha akaainisha kwamba   kama nchi,  Tanzania inakabiliwa na  changamoto mbili kwa pamoja. Changamoto hizo ni kukabiliana kwanza, na magonjwa yasiyo ambukizi na ya pili ni kukabiliana na magonjwa ambukizi.

Kutokana na changamozo hizo,  Waziri Duni anasema kuwa si vema  basi  aina moja ya ugonjwa ikatiliwa mkazo na kupewa kipaumbele dhidi ya  ugonjwa mwingine kwa kuwa yote yanashabihiana.

Aidha amezitaja changamoto nyingine zinazoikabili Tanzania  kuwa ni  ongezeko la kansa ya shingo  ya uzazi, ongezeko la wagonjwa wa kisukari wa asilimia tano, uvutaji wa sigara kwa asilimia 10,  ongezeko la watu wenye utizo wa kupita kiasi, unywaji wa pombe na maelfu ya watoto wanaozaliwa wakiwa na  matatizo ya  sickle –cell kila mwaka.

Mwishoni wa Mkutano huo, viongozi wa kuu wa nchi na serikali walipitisha tamkio la kisiasa ambalo  licha  ya kukiri kwamba magonjwa  hayo manne ni changamoto ya katika karne ya 21.Pia wamemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Mtendaji Mkuu wa  Shirika la Afya Duniani  ( WHO)na wadau wengine kuandaa taarifa itakayowasilishwa kwa viongozi hao katika Mkutano Mkuu wa 67 wa Umoja wa Mataifa.

IMETOLEWA NA  MAURA MWINGIRA
UBALOZI WA TANZANIA UMOJA WA MATAIFA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...