Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ally Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mapambano dhidi ya  ukatili kwa watoto,Marta Santos Pais aliemtembelea ofisini kwake leo na kuzungumza nae.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ally Iddi (katikati) na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mapambano dhidi ya  ukatili kwa watoto,Marta Santos Pais (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pamoja na ujumbe alioongozana nao Mwakilishi huyo.


Ipo haja kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Kuangalia uwezekano wa kuanzisha mafunzo maalum kwa  wanafunzi Maskulini ambayo yatasaidia elimu ya kujikinga dhidi ya udhalilishaji wa kijinsia.  

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mapambano dhidi ya  ukatili kwa watoto Bibi Marta Santos Pais  ametoa ushauri huo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  hapo Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. 

Bibi Marta amesema udhalilishaji wa Kijinsia  hasa kwa watoto wadogo unaathiri ustawishaji wa watoto hao jambo ambalo kama hakukuandaliwa mipango madhubuti hasa ya kielimu ongezeko  la vitendo hivyo litazidi. 

Amesema umoja wa Mtaifa Kupitia Shirika lake la Kuhudumia watoto la UNICEF utajitahidi kuendelea kutoa misaada ili kukomesha vitendo hivyo  vinavyokwenda kinyume na Haki za Binaadamu. 

Bibi Marta ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake wa kuyaweka makundi ya vijana, Wanawake na Watoto katika Wizara moja. Amesem jambo hilo litasaidia kuratibu mwenendo mzima wa makundi hayo katika kuyapatia huduma zinazostahili. 

Akitoa shukrani zake kwa juhudi za Umoja wa Mtaifa  katika kusaidia Maendeleo ya Zanzibar Balozi Seif amesemA Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuhakikisha tabia ya udhalilishwaji wa watoto nchini inapigwa vita na jamii yote. 

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amekutana na Balozi wa Japan Nchini Tanzania bwana Safaguchi aliyefika Ofisini kwake kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi Nchini Tanzania. 

Balozi Seif Ameipongeza Japan kwa kuwa Mshirika wa karibu wa  Tanzania katika kusaidia maendeleo ya Jamii hasa katika masuala ya maji na elimu yaliyopelekea kupunguza matatizo kadhaa yanayowakabili Wananchi.

 Naye Balozi wa Japan Nchini   Bwana Safaguchi  amezipongeza jitihada za Viongozi wa Tanzania zilizopelekea  kutekelezwa vyema majukumu yake. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...