Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha Agape Television (ATV) Dk. Vernon Fernandes akimuonyesha waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kushoto) Dk. Emmanuel Nchimbi jinsi satellite dish inavyosaidia kurusha matangazo nyumba hadi nyumba na kuwawezesha wananchi waliopo vijijini kupata matangazo yao. Waziri Dk. Nchimbi alitembelea kituo hicho kilichopo Mbezi jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuona utendaji kazi na kuimarisha mahusiano ya kikazi baina yao.
Mkurugenzi wa vipindi wa kituo cha Agape Television (ATV) Dk. Anny Fernandes akimkabidhi zawadi ya king’amuzi cha Tanzania Integrated Network Grid (TING) waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi mara baada ya waziri huyo kumaliza kutembelea kituo hicho. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ATV Dk. Vernon Fernandes.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha Agape Television (ATV) Dk. Vernon Fernandes akimueleza waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kushoto) Dk. Emmanuel Nchimbi maana ya neno TING lililoandika juu ya ving’amuzi vyao ambayo ni Tanzania Integrated Network Grid. Waziri huyo alitembelea kituo hicho kilichopo Mbezi jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuona utendaji kazi na kuimarisha mahusiano ya kikazi baina yao. Kulia ni Muuzaji msaidizi wa ving’amuzi hivyo Beatrice Mulinda.
Mkurugenzi wa vipindi wa kituo cha Agape Television (ATV) Dk. Anny Fernandes akimuonyesha waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kushoto) Dk. Emmanuel Nchimbi barua mbalimbali za watazamaji wa Runinga hiyo ambao wanazituma kwa ajili ya kufanyiwa maombi kutokana na matatizo mbalimbali yanayowasumbua . Kulia kwa Anny ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ATV Dk. Vernon Fernandes akifuatiwa na Wilfred Kanyana ambaye ni Meneja.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha Agape Television (ATV) Dk. Vernon Fernandes akimuonyesha waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kushoto) Dk. Emmanuel Nchimbi jinsi vipindi mbalimbali vinavyoandalia katika kituo hicho. Waziri Dk. Nchimbi alitembelea kituo hicho kilichopo Mbezi jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuona utendaji kazi na kuimarisha mahusiano ya kikazi baina yao.
Fundi mitambo wa kituo cha Agape Television (ATV) Daudi Mkwela akimuonyesha waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kushoto) Dk. Emmanuel Nchimbi jinsi mitambo ya digital na analogy inavyofanya kazi. Waziri Dk. Nchimbi alitembelea kituo hicho kilichopo Mbezi jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuona utendaji kazi na kuimarisha mahusiano ya kikazi baina yao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha Agape Television (ATV) Dk. Vernon Fernandes akimuonyesha moja ya studio zao waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) wakati alipotembelea kituo hicho kilichopo Mbezi jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuona utendaji kazi na kuimarisha mahusiano baina yao.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...