Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini imetoa ufafanuzi kufuatia Kimbunga kilichoambatana na Mvua kali na kusababisha Nyumba zaidi ya 90 kuezuliwa Mapaa yake huko Mbagala eneo la Mangaya katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Hali ya Hewa Dokta  Hamza Kaberwa ameiambia Uhuru FM leo kuwa hali hiyo ya Kimbunga inatokana na mabadiliko madogo ya Ardhi katika Bahari ya Hindi.

Kimbunga hicho kilichoambatana na Mvua pia kimesababisha watu Wanne kujeruhiwa vibaya.

Kufuatia hali hiyo imesema mabadiliko hayo yametoka Baharini kuelekea Pwani ya Dar es salaam kwa umbali wa Kilometa Mbili hadi Tano na hivyo kusababisha Kimbunga hicho kilichoambatana na Mvua.

Pamoja na mambo mengine Mamlaka hiyo ya Hali ya Hewa imetoa tahadhari kwa wananchi kuwa Mvua za Vuli zitakuwa Juu ya Wastani katika eneo la Kaskazini ikiwemo Dar es salaam hivyo wananchi wachukue tahadhari za kukabiliana na hali hiyo hususani wananchi wanaoishi Mabondeni.

Wakati huo huo, Mvua hizo pia zimesababisha Mifereji ya Maji Taka kujaa na kusababisha Maji Taka kusambaa katika barabara na maeneo kadhaa ya Jiji la Dar es salaam hatua iliyoleta usumbufu kwa wananchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...