Katika zama hizi za utandawazi na muingiliano baina ya tamaduni zetu za asili na tamaduni za kimagharibi, imekuwa ni kawaida kwa vijana wa rika tofauti na jinsia zote kutoga ulimi, mdomo, kitovu ama kivimbe cha nyusi kwa sababu tofauti tofauti sana.
Hivyo basi, ni muhimu sana kufahama ukweli kuhusu faida ama hasara za kutoga ulimi ama mdomo kabla hujatekeleza azma yako ya kutoga viungo hivi vya mwili.
Kutoga Ulimi ama Mdomo kunaweza kukusababishia madhara yasiyotarajiwa
Matokeo mazuri zaidi ya kutoga ulimi ama mdomo ni kutokutokea kwa kidonda ama kivimbe, wakati matokeo mabaya kutokea kwa baadhi ya watu ni pamoja na kuvunjika kwa meno/jino, kuvuja kiasi kikubwa cha damu, ama maambukuzi ya bakteria kwenye kidonda. Kutoga ulimi hujumuisha kutumika kwa sindano inayopenyezwa katikati ulimi ili kupitisha na kuhifadhi kipini, ama ndoana ama hereni ya urembo. Kazi hii ya kutoga ulimi mara nyingi ganzi huwa haitumiki. Baada ya kutoga, kuvimba kwa ulimi na maumivu ya muda hutokea.
Madhara ya kutoga Ulimi
Kutoga Mdomo
Kutoga mdomo ni pale pete ya urembo inapovalishwa ama kuhifadhiwa ndani ya mdomo. Majeraha ya kutoga mdomo hupona haraka zaidi, hata hivyo unapaswa kutunza kidonda cha jeraha hili kwa umakini
mkubwa wakati wa kupona. Vyakula, vinywaji na moshi wa sigara vinapofikia kidonda hiki, vinaongeza hatari ya kupata maambukizi kwenye kidonda.
Kishikizo vishikizo vya pete hii ya urembo kinaweza kusababisha vidonda kwenye fizi ama kuharibu jino. Kwa baadhi ya watu, tiba ya kupandikiza fizi hutumika kurejesha fizi zilizoathirika. Kama ilivyo kwa kutoga ulimi, kutoga mdomo pia kunaweza kuathiri mshipa wa fahamu hivyo kuathiri mienendo ya misuli ya kwenye eneo la kinywa na mdomo.
Je, una mpango wa kutoga Ulimi ama Mdomo?
Ikiwa unapanga kutoga viungo hivi vya mwili, unashauriwa ufanye mambo yafuatayo yatakayo kuwezesha kupata huduma ambayo haita athiri afya yako:
Hii ni mitindo ya Ughaibuni ambayo huko kuna mazingira tafauti na TZ kama vile matibabu, hali ya hewa na fedha.
ReplyDeleteSasa mimi ni mmakonde na ninataka kutoga lakini sitaki kutmia vyuma anataka mti wa mpingo ambao ndio asili yetu sisi pia huo ni hatari?
ReplyDelete