Waziri wa Uchukuzi Mhe.Omar Rashidi Nundu,ametoa salamu za Rambi Rambi kutokana na vifo vya watu zaidi ya 200 vilivyotokea katika eneo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyotokana na kuzama kwa Meli ya Mv Spice .
Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya  habari  kwa  niaba ya Katibu Mkuu Edward  Mkiaru, Waziri Nundu alisema, Wizara imepokea taarifa hiyo kwa masikitiko na inawapa pole wafiwa wote pamoja na kuwaombea afya njema wale wote  walionusurika katika ajali hiyo.
Aidha wizara imewashukuru wananchi wote walioshiriki kwa njia moja ama nyingine katika kuokoa wale waliofikwa na mkasa huo.
“Kutokana na tukio hili tunamuomba Mwenyezi Mungu awafariji wote waliofikwa  katika kipindi hiki kigumu na pia azilaze roho za Marehemu wa ajali hiyo mahali pema peponi”alisema Mkiaru

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivi NI Vichekesho sana:

    Waziri anatoa Rambi Rambi kwa Niaba ya Katibu Mkuu?; Yeye ni waziri na ni yeye anaetakiwa kuwa mbele; What is wrong with this people ?

    Kutokana na tukio hilo anamuomba mungu? Alitakiwa aseme kutokana na Tukio hili anajiuzulu; What is wrong with Tanzanian Leaders ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...