Kwa niaba ya wana Jumuiya ya Watanzania nchini Misri (TSE) kueleza masikitiko yetu ya uchungu mkubwa kufatia na msiba mzito wa kuzama kwa meli ya “MV Spice Islander” siku chache zilizopita na kupoteza maisha ndugu na jamaa marafiki na wapendwa na wengine kujeruhiwa. Tunatoa rambirambi kwako wewe Mh. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa rais wa Zanzibar Mh.Dr.Ali Mohamed Shein na balaza la mapinduzi Zanzibar na family ya wafiwa na majeruhi.
Kwa niaba ya Jumuiya ya (TSE) tungeomba mpokee salaam zetu za rambirambi na pole kwa ndugu jamaa na marafiki zetu wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa msiba huu mzito.
Pia bila ya kuwasahau kwa kuwashukuru na pongezi kubwa kwa wote waliojitokeza kufanikisha uokoaji na uopoaji wa maiti na waliotoa msaada wa hali namali.
Mwenyeezi Mungu awarehemu awasamehe makosa yao na awalaze mahali pema peponi. Na walionusurika Allah awaponye awape moyo wa subira na urahisi wa matakwa yao. (Amin)
Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania nchini Misri
Abdallah Daruweshi
Cairo
12 September 2011
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...