JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA IMEZIPOKEA TAARIFA ZA AJALI YA MELI ILIYOKUWA IKISAFIRI KUELEKEA PEMBA KWA MASIKITIKO MAKUBWA. TUNAUNGANA NA WATANZANIA WOTE HUKO NYUMBANI NA NJE KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA HUU WA TAIFA.
MWENYEZIMUNGU AWAREHEMU WOTE WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI.
PIA TUNAPENDA KUWATANGAZIA WATANZANIA WOTE WANAOISHI ITALY KUWA SIKU YA JUMATANO KUTAKUWA NA MKUTANO WA WATANZANIA WOTE KWA AJILI YA KUTOA HESHIMA ZETU NA KUITISHA HARAMBEE YA MICHANGO KUCHANGIA MSIBA WA TAIFA LETU. MKUTANO UTAFANYIKA SAA KUMI NA MOJA NA NUSU TAFADHALI MAHUDHURIO NI LAZIMA KWA KILA MTANZANIA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA!!
Abdulrahamani A.Alli
Mwenyekiti
JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA..
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...