Kwa heshima, taadhima na unyenyekevu mkubwa tunapenda kuwakumbusha kwamba Septemba 8, 2011 Michuzi Blog inatimiza miaka sita toka kuzaliwa kwake kule Helsinki, Finland, siku kama hii.
Awali ya yote tunapenda kutoa shukurani zetu nyingi kwenu nyie wote, bila kujali wapi ulipo ama umekuwa ukitembelea Globu ya Jamii kuanzia lini, kwani sapoti yenu iwe kwa uchache ama kwa uwingi ina maana kubwa sana sana kwa timu nzima ya Michuzi Blog.
Katika kuadhimisha siku hii adhimu, ambayo kwa bahati mbaya hatutoiadhimisha kwa sherehe za aina yoyote kutokana na mambo yaliyo nje ya uwezo wetu na mikononi mwa Mola, ni vigumu kumtaja kila mmoja wenu kwa jina kwa msaada na sapoti mliyotupa muda wote huu.
Pamoja na hivyo, tunaomba kwa unyenyekevu mkubwa tuwataje wachache ambao sio tu watawakilisha kadamnasi nzima, bali pia michango yao imekuwa chachu kwa uhai wa Michuzi Blog ambayo kwa matakwa yake MAANANI inaendelea na Libeneke kama imeanza jana, na kubwa hapa ni kuaminiwa na wewe mdau kwa asilimia kubwa.
Tunaomba tuanze na Kaka Ndesanjo Macha, aliyembatiza Ankal katika fani hii. Bila yeye na Ankal kukutana na kubadilishana mawazo pale Finlandia Hall jijini Helsinki Septemba 8, 2005, Globu ya Jamii isingezaliwa. Pamoja naye tunamshukuru sana sana kaka Fidelis Tungaraza 'Mti Mkubwa', ambaye ni mdau wa kwanza kuchangia mawazo na hekima katika kufanikisha hiki kidogo tulichonacho. Mbarikiwe sana Fide na Ndesanjo.
Shukrani zetu nyingi ziende kwa Benki ya CRDB ambayo ilikuwa ya kwanza kuona umuhimu wetu na kutudhamini kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 2007. Bila CRDB uwezekano wa kupata wadhamini wengine ungekuchua muda sana, kwani ni wachache walioona umuhimu wa kusaidia katika hili. Asante sana CRDB.
Shukrani za pekee ziwaendee MK COMPUTER TWEAKS ambao ni wabunifu wa Globu ya Jamii. Yaani, Hiki unachoona hapa kimesababishwa na wao. Ahsante sana sana Christopher Makwaia. Hatuna la kusema zaidi ya shukrani hizi. Ubarikiwe kaka.
Tutakuwa watovu wa fadhila kama kwa kipekee kabisa tusipoitaja VODACOM TANZANIA kwa kuwa wafadhili wetu wakuu kwa miaka mitano mfululizo. Hakika ufadhili wa kampuni hii pendwa ya mawasiliano imefanikisha mengi ya Globu ya Jamii kiasi hata tukiorodhesha fadhila zote ilizotupatia itachukua ukurasa wote huu na bado tusiwe tumetaja robo tu ya fadhila hizo. Asante sana VODACOM. Tunawashukuru, tuwawapenda na tunawaheshimu mno.
TANZANIA BREWERIES LIMITED (TBL) pia mmekuwa wahisani wetu wakubwa kwa muda usiopungua miaka minne sasa, ambapo mchango wenu kwetu na jamii kwa jumla ni wa kuigwa. Azma yenu ya kutimiza maana halisi ya social responsibility daima itakuwa mioyoni mwetu. Kupitia kilaji chenu pendwa cha NDOVU PREMIUM LAGER hakika tumeweza kufika hapa tulipo leo. Asante sana TBL.
Bila kumaanisha umuhimu mkubwa ama mdogo katika uhisani, wapendwa wahisani wengine ambao shukrani zetu twazituma ni pamoja na Benki ya Jamii ya NMB, Benki mama ya mabenki nchini ya NBC, Shirika la mfano la ndege la PRECISION AIR, kampuni inayoongoza kwa usafiri ya SKYLINK TOURS AND TRAVEL , Kiota cha maraha na ukarimu wa Mtanzania cha GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL na wengine wote wanaotufadhili.
Pia tunapenda kutoa shukrani kwa wakuu na watendaji wanaotupa moyo na sapoti kila kukicha wa a Ikulu za Dar es salaam na Zanzibar, Mawaziri, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kusahau Taasisi za Serikali na za binafsi. Tunashukuru sana, sana sana waheshimiwa.
Shukurani za ziada ziawaendee pia wawakilishi wetu nchini na nje ya nchi. Hapa nyumbani tuna furaha na fahari kuwataja Jeff Msangi wa BongoCelebrity, Ahmad Michuzi wa JIACHIE BLOG, Othman Michuzi wa MTAA KWA MTAA BLOG, Woinde Shizza na Dickson Busagaga wawakilishi wetu Kanda ya Kaskazini, Audax Mutiganzi wa Kanda ya Ziwa, John Nditi wa Morogoro, Muhidin Amri wa Kanda ya Kusini, Francis Godwin wa Iringa, G. Sengo wa Mwanza, MBEYA YETU BLOG wa Mbeya na wengine wote mnaotusaidia.
Ughaibuni nianze na Kamanda wa FFU Ras Makunja wa Ujerumani na kundi lake kabambe la Ngoma Afrika, DJ Luke Joe wa VIJIMAMBO wa Washington DC, kaka Abou Faraji wa TZ UK London, Freddy Macha wa London, kaka Frank Eyembe na kikosi kazi chake cha Urban Pulse cha Reading, UK, Sporah Njau wa London, Jestina George wa London, Da’Chemi Chemponda na Da’Subi wa Marekani na wote wengine.
Kama mnavyoona orodha ni ndefu sana, kiasi ya kwamba hatuna budi kuwataka radhi wale wote ambao hatukuwataja kwa majina ama nafasi zao. Tunaomba itoshe tu kwa kusema wote tunawapenda, tunawashukuru na kuwajali.
Mwisho ni shukurani kwa walezi wetu ambao kwa kweli tunajihisi ni wenye bahati kubwa kupata Baraka zao kila siku.Mh JK tunakushukuru kwa yote. Mzee Benjamin Mkapa na Alhaj Ali Hassan Mwinyi tunawaombea maisha marefu, maana misaada yenu ya mawazo kupitia wasaidizi wenu ni hazina kwetu. Dr Asha-Rose Migiro (ulikuwapo Helsinki Michuzi Blog ilipozaliwa)Ubarikiwe kwa yote. Balozi Mwanaidi-Sinare Maajar, Balozi Peter Kallaghe na naibu Balozi Chabaka Kilumanga na Balozi Mohamed Maharage tunaona fahari na heshima ya kipekee kuwa karibu nanyi. Profesa Mark Mwandosya na Mama Lucy Mwandosya tunakushukuru na tunakuombea Mola akupe ahueni huko uliko. Dr Emmanuel Nchimbi ahsante sana sana. Mh Sethi Kamuhanda asante sana kwa kutupa faraja na moyo. Mh Freeman Mbowe, Mh Zitto Kabwe tunashukuru kwa kutuunga mkono. Kaka Eric shigongo na vijana wako tunashukuru mno kuwa karibu nasi. Dada Regina Mengi ushauri wako tunauenzi daima.
Tunaomba tusishie hapa kwani orodha ni ndefu mno.
-MICHUZI
Congrats.
ReplyDeleteUS Blogger
Ni miaka sita ya kazi njema kwa jamii. HONGERA SANA KAKA MICHUZI!
ReplyDeleteMaggid,
Iringa.
"Happy b.day 2 u".Sasa Ankal unaonaje ukatuwekea na PICHA za wafanyakazi wa blog yetu na wasifu mfupi tu manake mnafanya kazi nzuri.Ni mawazo yangu tu
ReplyDeleteDavid V
Congratulations Mzee wa libeneke; kazi nzuri sana;
ReplyDeleteMdau, Mkuu wa DC
Iddi Sandaly
NDUGU MICHUZI TUNASHUKRU KWA YOTE MNAYOTUFANYIA YA KUTUUNGANISHA NA NDUGU WATANZANIA KATIKA MTANDAO HUU PIA NAWATAKIA KILA LA KHERI KATIKA KUFIKISHA MIAKA 6 NAWAOMBEA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI NDEFU.
ReplyDeletePIA NAKUOMBA ILI KUINUA UCHUMI WA NCHI YETU WASILIANA NA STATION ZA TV TANZANIA ILI WAWASILIANA NA UBALOZI WA MISRI HAPO TANZANIA WAWEZE KUTUMIA ARAB NA NILE SATI ILI KUITANGANZA TANZANIA KATIKA DUNIA HII ITAKUWA UMEISADIA NCHI NZIMA KATIKA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA NA PIA WATANZANIA.
TANZANIA NI NCHI YENYE NEEMA NYINGI TATIZO HAIJULIKANI KABISA WEWE CHUKULIA ETHIOPIA, ERITRIA, CHAD, SUDAN KUSINI NA NYINGI ZINARUSHA MATANGANZO YAO KWA KUTUMIA NILE NA ARAB SATI WAMEONGEZA SANA PATO LA NCHI.
KWA MFANO UTURUKI KIASI YA MWAKA WAMEANZA KUTUMIA ARAB NA NILE SATI PATO LAO LIMEONGEZEKA MARA 3 KATIKA NCHI ZA MASHARIKI YA KATI.
NAIMANI TANZANIA TUNA VIVUTIO VINGI SANA MBUGA ZA WANAYAMA, MITO, ZANZIBAR NI MAMBO MENGI.
HIVYO KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 6 IKIBIDI WASILIANA HATA NA RAISI ILI KUWEZA KUOMBA UBALOZI WA MISRI TANZANIA KUSAIDIA KURUHUSU TANZANIA CHANNELS ZOTE ZA TV KURUSHA KUPITIA HIZI ARAB NA NILE SATI.
SHUKRANI SANA
ANKAL, HONGERA SAAAAAANA KWA KUTIMIZA MIAKA SITA YA MICHUZI BLOGU YA JAMII. BILA KUSOMA YALIYOJIRI KILA SIKU DUNIANI (HUSUSANI NYUMBANI TANZANIA) KUPITIA BLOGU YA JAMII HUWA SIPATI USINGIZI. NAITAKIA BLOGU YA JAMII 6TH ANNIVERSARY NJEMA. ALUTA KONTINUA!!!!!!!!!!!!, DR. MWITA, LONDON
ReplyDeleteIngawa leo bado tarehe 5 na sio 8, pokeeni wote mliotajwa hongera zangu. Kwa kipindi kifupi hii blog imekuwa kama uso wa blogs za Tz. Mie binafsi bila undugu wala kufaamiana, mara kadhaa niliomba na kuwekewa missada ktk tutaaz na kumbukumbu za waliotutangulia. Shukrani kwa kutupatia news na kutupost pale tunapoomba. Karibu sana Eastern Block!
ReplyDeleteBlackmpingo
tunaitakia blog ya jamii maisha mema na marefu,iweze kutupatia habari usiku na mchana 24/7,
ReplyDeletePia tunawatakia afya njema na uvumilivu timu yote na uongozi wa blog ya jamii.
wadau
FFU UGHAIBUNI
Happy birthday to michuzi.blogspot.com. Ankal, ahsante sana kwa kutupasha habari ju matukio mbalimbali katika nyanja tofauti. All the best. Mdau.
ReplyDeleteHongera na pongezi bro Issa. Nawatakia wewe, familia yako na wasomaji wako wote kila la heri.
ReplyDeleteHappy Birthday Michuzi Blog. Nakupongeza sana Ankal kwa kuanzisha chombo hiki ambacho kinatuhabarisha na kutupatia elimu, burudani pia. Mimi naitwa Jerome J. Kamuhangire, naishi Dubai, haipiti siku bila kusoma Michuzi Blog, kwani ndipo ninapopata habari na matukio "live" yanayoendelea huko nyumbani na dunia kote. Mungu akuongezee uwezo na upeo wa kukikuza chombo hiki.
ReplyDeleteJerome J. Kamuhangire
Kempinski Hotel Ajman, Dubai UAE.
E-mail: jeromekamuhangire@hotmail.com
Tel. +971 56 730 5 780
nikupongeze michuzi kwa kutimiza miaka hiyo ninaamnini kwamba umekutana na changamoto nyingi sana lakini uvumilivu na kujipa moyo na kuzingatia ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali umeweza kuendelea na kuwahabarisha watu. Ninakuombea kila kheri katika yote ili tuweze kuisaidia jamii kwa njia hizi za mitandao na Mungu aipandishe Tanzania katika viwango vya hali ya juu
ReplyDeleteNdimi
Johnson Jabir
Blogger wa blogu ya JAIZMELA
Mbona leo ni tarehe 5 na wewe unasema blog imeanza tar 8? ati ankal...mbona changanya mambo hapa..
ReplyDeleteMIAKA SITA DUH! Ni mingi kaka M..HONGERA SANA KWA KAZI UNAYOIFANYA NA PIA HONGERA SANA KWA KUTIMIZA MIAKA 6.
ReplyDeleteMuhidin,
ReplyDeleteHuwezi kuamini!? Jana minara ya saa moja jioni nilivinjali Finlandia Talo jengo ilipozaliwa issamichuzi blogspot. Mawazo yakanijia kama ninapopita Mtaa wa Lumumba pale kwenye jengo kilipozaliwa chama cha TANU na kusoma yale maandishi " Hapa ndipo kilipozaliwa Chama cha TANU"! Nikasema "Hapa ndipo ilipozaliwa issamichuzi blogspot". Nikakukumbuka na kumkumbuka Ndesanjo na issamichuzi blogspot.
Ndani ya jengo lile lile ndipo Marehemu Mwalimu Hukwe Ubi Zawosse aliposimikwa Shahada ya Udaktari wa Heshima na Chuo cha Muziki cha Sibelius. Tulishuhudia hafla ile kwa shangwe kubwa mno na kuimba nyimbo za taifa za Tanzania na Finland na kuziona bendera za Tanzania na Finland zikiwa zimepandishwa mbele ya jengo la Finlandia.
Mkuu,
Nikianza huwa simalizi. Hongera sana kwa kutimiza miaka minane. Mwenyezi Mungu akubariki siha ya mwili na akili. Amen.
Rafiki yako,
Fidelis M Tungaraza.
Hongera sana Michuzi na Blog ya Jamii kwa kazi njema.
ReplyDeleteAnkal kwa kweli sisi Timu nzima ya Mbeya Yetu Blog tukiwa tunaongozwa na Fredy Tony Njeje Hatuna neno zaidi ya kukushukuru sana kwa msaada mkubwa ambao umetupa mpaka Kuifikisha Blogu Dada ya Jamii kufikia mpaka hapa ilipo sasa, Tunakutakia maisha Mema Mwenyezi Mungu akuongezee zaidi na zaidi. Pia na kwa Timu nzima ya Globu ya jamii.
ReplyDeleteFredy Tony Njeje
Mbeya Yetu Blog
Hongera sana Ankal...endelea kupiga hatua kwa ubunifu
ReplyDeleteHongera sana. Nakutakia kila la heri wewe na familia yako, wafadhili na wasomaji wa blog yako.
ReplyDeleteMimi mbona umenisahau?
ReplyDeleteAnon wa Mon Sep 05, 04:15:oo PM 2011, Hatujakusahau. Kwa hivyo na wewe hongera kwa kuwa msomaji wetu japo hujatoa jina lako...ha ha ha ...
ReplyDeleteHongera sana blog ya jamii mr.Michuzi,tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu
ReplyDeleteuendelee na Libeneke.
Mdau Vumbi Dekula
S W E D E N
Many Congrats and thanks for all the love & support. God bless you and all of us as we continue rolling the blogging ball. Happy Birthday Michuzi Blog
ReplyDeleteHongera sana Ankal kwa kazi nzuri kila siku na kwakutoa fursa kwa bloggers wengine kuonekana kwa kupitia jukwaa lako.
ReplyDeleteMchango wako ktk kuiinua Tembeatz.blogspot.com unatambulika
tembeatz.blogspot.com