Wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya wanawake 'Twiga Stars' wakiwa kapika picha ya pamoja na wenzao wa timu ya taifa ya netiboli Taifa Queens pamoja na viongozi wao.
Wachezaji wa timu ya taifa ya netiboli Taifa Queens wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CHANETA mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea Maputo Msumbiji. Timu hiyo ilipata medali ya fedha.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi akizungumza katika hafla ya kuwakaribisha wachezaji walioshiriki mashindano ya All Africans Games.
Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi akizungumza wakati wa hafla ya kuwakaribisha wachezaji walioshiriki mashindano ya All Africans Games. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Chaneta, Rose Mkisi na Kocha Msaidizi wa Twiga Stars, Nasra Mohamed.
Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa TFF,Angerile Osiah pamoja na Katibu Mkuu wa BFT, Makole Mashaga.
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Wanawake ‘Twiga Stars’ Charles Boniface Mkwasa akizungumza na mchezaji wa Twiga Stars, Fatuma Abushir pamoja Mwenyekiti wa Soka ya Wanawake, Lina Mhando.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Wanawake Twiga Stars wakipata chakula katika hafla ya kuwakaribisha.Picha na Francis Dande.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...