Na Woinde Shizza,Arusha

WAHITIMU wa kidato cha Nne mkoani hapa wameitaka serikali kushughulikia haraka suala la upatikanaji wa umeme wa uhakika kutokana na umuhimu wake kijamii na kiuchumi.

Wakizungumza katika lisala yao wakati wa mahafali ya kumaliza kidato cha Nne, wahitimu kutoka shule ya Fikiria Kwanza walisema kuwa swala la umeme limekuwa tatizo kubwa sana kwani limewaathiri katika masomo yao .

Mmoja wa wahitimu hao,Anna Estomi,alisema kuwa wamekuwa wakipata wakati mgumu sana wakati wanataka kusoma usiku kutokana na kukosa umeme pia walibainisha kuwa wamekuwa wakitumia mishumaa kusomea ambapo inaleta madhara makubwa hapo baadae.

Alisema kuwa mbali na wao wanafunzi kupata tabu kutokana na swala hili pia ukosekanaji wa umeme umesababisha uchumi wa nchi kushuka kwa kiasi kikubwa .

“Unajua swala hili la umeme limewaathiri watu wengi mbali na sisi wanafunzi pia wafanyabiashara ambao ni wadogo wadogo ambao wanategemea umeme wamekuwa wanapata shida sana kwani wamekuwa wanashindwa kufanya kazi kwa wakati kutokana na kukosa umeme”alisema mmoja wa mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la Anna Estomi.

Aliongeza kuwa pia tatizo hili la umeme limekuwa likiwaathiri pia vijana wengi ambao walikuwa wanafanya kazi katika makampuni yanayofanya kazi zake kwa kutegemea umeme pamoja na wale wa viwandani kwani wengi wao wameondolewa kazini kutokana na kutokuwepo na kazi.

Afisa Elimu na Taaluma kwa shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Dainesi Mosha aliwapongeza wanafunzi hao pia pamoja na walimu kwa jinsi walivyoweza kushirikiana hadi hapo walipofika.

Aliitaka serekali kuwaangaliwa walimu sana kwani bila walimu hamna kitu ambacho kingefanyika huku akisema kuwa serekali ainabudi kuwahudumia walimu vizuri na kuwathamini kwani wanafanya kazi kubwa sana ya kuwaondoa watu ujinga.

Pia aliwataka waajiri wa shule mbalimbali kuajiri walimu ambao wanataaluma ya kutosha katika fani na sio kuwachukuwa walimu wa mitaani ambao hawana elimu ya kutosha ya kufundisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nunua kibatari na mchana usizembee!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...