Na Tiganya Vincent - MAELEZO-Dar es salaam
Chama cha Wanasheria cha Tanzania Bara (TLS) kimeenesha mafunzo ya kuwawezesha Watendaji Mtaa na Kata wa Wilaya ya Temeke na Kinondoni jinsi ya kutoa msaada wa kisheria kwa jamii anayoitumikia.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaa na Mratibu wa Mradi wa Maboresho wa Sekta ya Sheria kutoka TLS Maria Matui wakati anaongea waandishi wa habari.
Alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha watendaji hao kufikisha ujumbe wa msaada wa kisheria kwa wananchi ili waweze kutambua wapi wanaweza kupata huduma hiyo bila malipo.
Matui aliongeza kuwa mafunzo hayo yanawashirikisha watendaji 90 kutoka maeneo mbalimbali ya Wilayani Kinondoni na Temeke ili kuwajengea uwezo wa kuwaelimisha wananchi jinsi ya kupata msaada wa kisheria na vilevile wenyewe kutoa msaada huo pindi mwananchi anahitajika.
Alisema kuwa chini ya mafunzo hayo wananchi watapata ufahamu juu ya vigezo vinavyostahili mtu kupata msaada wa kisheria bila malipo kutoa TLS na pia kujua siku ya msaada wa kisheria kitaifa .
Matui alisema kuwa mwananchi wamekuwa hawapati huduma za msaada wa kisheria kwa sababu ya kushindwa kumudu gharama za mawakili na wakati mwingine baadhi ya maeneo hakuna mawakili hali inayowafanya kukosa haki zao za msingi.
Alisema mafunzo hayo yanakusudia kuhakikisha kuwa msaada wa kisheria unafika katika ngazi ya chini ya jamii kwa kuwawezesha wasaidizi wa kisheria kuweza kutambilika .
Chama cha Wanasheria Tanzania Bara(TLS) kinaendesha mafunzo hayo chini Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria(LSRP) wa Wizara ya Katiba na Sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...