Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanawake wa Korogwe kabla ya kuondoka kwenye makazi ya Mkuu wa wilaya hiyo jana. Alikwenda Korogwe kuhudhuria ibada ya kumweka wakfu askofu wa pili wa Dayosisi ya Tanga, Canon Maimbo William Mdolwa. (Picha na Ofisi ya Waziri MKuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Michuzi samahani sana, najua hii ni blog yako na utakalo ndio unaandika. Mara nyingi mimi husoma tu unachooandika bila ya kusema lolote hususan matumizi ya maneno, yaani nashindwa kutambua time ambayo unafanya mzaha au unapokuwa serious au unapokuwa umekusea kuandika.

    Hata hivyo leo nimeshindwa kujizuia na naomba unieleimishe nini unakusudia unaposema kumweka wakfu? nini wakfu kwa lugha ya kisasa? Maana nijuavyo mimi wakfu ni neno lenye asili ya kiarabu na ndio maana waislamu hufanay misikiti yao kuwa wakfu na pia kule zanzibar kuliwahi kuwepo na wizara ya wakfu na mali ya amana. Sasa imekuwaje kuwaje leo wakfu ikawa inahusishwa na dini ya kikiristo? Sitafuti ugomvi natafuta kuelimishwa.

    ReplyDelete
  2. Maneno mengi ya kiswahili yametokana na kiarabu na uhusiano huo si lazima uwe ni ukusiano na dini ya kiislamu. KUNA WAARABU WAKRISTO VILE VILE NA WANATUMIA MANENO HAYO HAYO. Vile vile kuna waarabu mabudha, wasio na dini, nakadhalika.

    Navyofahamu mimi "wakfu" ni kama "consecration" kwa kiingereza na maneno yahayotumika kiswahili ni "kusimika" au "wakfu" au yote kwa pamoja. Labda wengine wana mawazo mengine ila tu nadhani ni muhimu kutofautisha kiarabu kama lugha na dini ya kiislamu kama nilivyosema hapo awali.

    ReplyDelete
  3. Huyo jamaa ni mdini tu na wala hana lolote. Si kwamba alikuwa hajui nini maana ya wakfu ila anatafuta tu kuchokonoa mambo yasiyo ya msingi!

    ReplyDelete
  4. Wakfu ni sawa na Kusimika, Kusimikwa na kuwekwa Wakfu ni sawa, umetaka kuelimishwa, hiyo ni LUGHA tu imetumika na sio DINI. Dini ni Dini naLughani Gugha, amka wewe Anonymous namba moja!

    ReplyDelete
  5. Mwambieni aelewe sijui wa wapi huyo?
    Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!?

    ReplyDelete
  6. ndio tabu ya kuchukua vya watu sisi tulikuwa na dini zetu nzuri lakini ujinga wa waafrika tukaiga upumbavu wa wazungu na waarabu

    ReplyDelete
  7. anon wa seo 07, 12:15:00 AM 2011

    Ni lazima kuwa wewe ni mtu mwenye power fulani ambazo watu wengine hawana, nguvu ambazo unaweza kujua yalio ndani ya nyoyo za watu pamoja na nia zao.

    Vyenginevyo ungeliwezaje ku-conclude kuwa mdau wa mwanzo alieuliza maana ya neno wakfu kuwa ni mdini?

    Kuwa mstaarabu mtanzania mwenzagu na wape watu benefit of the doubt, usirupuke tu na ku-judge watu usiowajua kwa kusoma sentensi mbili tatu tu walizoandika hapa. You need to think out of the box.

    Nawe anon wa wed sep 07, 09:58:00 AM 2011 chukua ushauri huu pia.

    ReplyDelete
  8. Kuweka Wakfu, ninavyofahamu mimi neno lina maana ya "Kutakasa" au Consecration in English, to declare "holy". Kusimika ina maana ya to set up au kumweka mtu mkuu kwenye nafasi fulani, tayari kuanza mission. Neno hili linahusiana na dini, si uislam au ukristo tu, hata dini nyingine pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...