Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja akizungumza  wakati wa uzindua wa Kamati maalum ya kusimamia uagizaji wa nishati hiyo kwa pamoja. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Na Francis Dande wa Globu ya Jamii

Kamati hiyo inatoa fursa kwa wafanyabishara kuagiza mafuta kwa pamoja badala ya kutumia utaratibu wa zamani, wa kila mmoja kuagiza kwa wakati wake na kujipangia bei sokoni.
Kamati hiyo yenye wajumbe nane itaongozwa na Mwenyekiti Prosper Victus kutoka Wizara ya Nishati na Madini.Wengine ni pamoja na Salome Makange, Kapteni T. P. Massaro wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Charles J. Sangweni (TPDC) na Ayoub Mbowe wa Mamlaka ya Mapato (TRA), pamoja na Mhandisi Saad S. Y. Fungafunga wa Wizara ya Uchukuzi.


Serikali pia imewateua, Joseph Haule (Wizara ya Ujenzi), na Shogholo Msangi kutoka Wizara ya Fedha, kuwa katika Kamati hiyo ambayo itaanza kufanyakazi mara moja.


Akizungumza katika mkutano wa pamoja na wadau wa mafuta uliyofanyika leo katika hoteli ya Movinpick jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema wafanyabiashara wanawajibu wa kuifuata na kuipa ushirikiano kamati hiyo.


Kwa mujibu Ngeleja mfanyabiashara yoyote atakaye kiuka au kutoifuata Kamati hiyo watalazimika kupewa adhabu ikiwemo kufungiwa kwa muda wa miaka 15.


“Serikali inasema kama makampuni yoyote yanayokaidi amri wafunge biashara na waondoke.. lazima sheria zifuatwe alisema Waziri Ngeleja


"…Mfanyabiashara yoyote atakayekiuka uundwaji wa Kamati hataruhusiwa kufanya biashara kwa muda wa miaka 15, kufutiwa leseni na kupigwa faini nyingine”alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...