Kaka Issa,
awali ya yote naomba upokee heshima yako,na wewe unipe heshima yangu.
Itifaki imezingatiwa!
Pili naomba nichukue muda huu kukupongeza wewe binafsi na wadau wa dawati la blogi yetu ya jamii hapo ofsini kwako,ninasema hongereni kwa kazi zenu nzuri tunazoziona.
Tatu naomba uendelee kunipa ruhusa niwapongeze wadau wa blogi yetu ya jamii popote pale walipo kwenye hii sayari ya dunia na mimi nikiwemo.Wadau hongereni sana kwa michango yenu katika tasia hii ya habari kupitia vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi yetu,mathalani blogi yetu hii ya jamii.
Kaka Issa wakati ninadodosa blogi yetu hii,nilikutana na habari iliyokuwa inatujuza wadau kuhusu blogi yetu kutimiza miaka sita toka kuhasisiwa kwake kule nchini Finland jijini Helsinki Septemba 8,2005.Mliokuwepo katika uhasisi huo hongereni sana kwani umhimu wenu haukuwa siku hiyo pekee,hadi leo unaonekana.
Kaka Issa,baada ya utangulizi huo wa dhati ya kweli naomba nijirejeshe kwenye hoja yangu kuntu iliyonipa moyo wa kukuandikia huu ujumbe na wadau kwa ujumla.
Binafsi nimekuwa na pendekezo la kuboresha jina la blogi yetu ya jamii kama ifuatavyo kaka Issa.
Badala ya kuiita blogi yetu ya jamii MICHUZI BLOG,nilikuwa napendekeza tuiite GLOBAL BLOG [GB '11] kufuatana na miaka itakavyokuwa ikiendelea.Kwa hali hiyo mwaka 2012,tutakuwa tukiiita GLOBAL BLOG[GB'12]......toka siku itakapo timiza miaka 6 ya kuhasisiwa mwezi huu.
Kaka Issa,na wadau kwa ujumla mtaniuliza,dhana ya kubadilisha jina imeanzia wapi na imekujaje hapa?na dhima yake hasa ni nini?
Mantiki ya kuiita Global Blog [GB'11],inashabihiiana na mawazo yafuatayo;
1.Kuifanya blogi hii iwe na mtizamo wa kisasa kwa watumiaji mbalimbali ulimwenguni kote-kwani ipo uwanda wa kimataifa kwa sasa.
2.Kuwahamasisha watumiaji kutoka pande zote za dunia kupata na kutoa taarifa za kitaifa na kimataifa kwa usahihi na kwa muda muafaka bila kujali mtumiaji ni wa asili gani kupitia blogi yetu hii.
3.Kukubaliana na mabadiliko yanayoendelea kujitokeza katika tasia ya habari kupitia blogi hususani linapokuja suala la ubunifu.
4.Kuwahamasisha wadau mbalimbali hususani wasio jua lugha ya Kiswahili kushiriki katika kutoa michango yao ya hali na mali ndani ya nchi yetu kupitia habari juu ya blogi yetu hii.Kuna wadau wa nchi za Mashariki ya Kati,wanahitaji kutujuza ya huko kwao kupitia blogi yetu hii.
5.Kukupa nafasi wewe binafsi na sisi wazawa wote na Taifa letu kwa ujumla hali ya kuthaminiwa na kuheshimiwa kwa watumiaji wasio wazawa popote hapa duniani.
Kaka Issa,sambamba na mawazo haya,ninadhani ni muda muafaka sasa habari kupitia blogi yetu hii,ziendane na ushindani wa taarifa mhimu na bora katika karne hii ya utandawazi na uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari wenyewe.
Kimsingi kaka Issa na wadau wote,nisingependa kuwachosha kwenye suala la uhalisia kama hili.Ni imani yangu kuwa binafsi kama mdau wa Blogi ya jamii,nafasi yangu hii nimeitumia kama inavyotakiwa katika eneo lolote lenye tija kwa maendeleo ya watu.
Baada ya kuwashirikisha hayo wadau,naomba ruhusa yenu sasa nilejee kwenye majukumu mengine ya ujenzi wa Dunia.
Mwisho nawatakia wadau wote kila la kheli tunapokuwa tukielekea kusheherekea siku ya kuhasisiwa Michuzi blogi hapo kesho kutwa.
Naomba kuwasilisha!!
Mdau Mashariki ya mbali.
J.K Junior!
-----------------------------------
Mdau JK Junior!
Awali ya yote timu nzima ya Globu ya Jamii inakupa shukrani nyingi mno kwa kuchukua wasaa na kutuletea wazo lako kama ilivyoanishwa hapo juu. Kwa kweli tumehemewa na tunalichukulia hilo wazo kwa uzito mkubwa stahili. Ila kama ujuavyo sisi ni watumishi wenu, neno lenu ni amri kwetu. Hivyo tunahisi itakuwa busara turuhusu wadau wachangie mawazo juu ya wazo lako hilo. Sisi hatubagui na wala hatuchagui, kwani atayetuzika hatumjui. Hivyo wadau popote mlipo, baada ya kusoma Wazo la mdau JK Junior, nini usemi wenu ama wazo lenu katika hili?
Libeneke Oye!
Michuzi
Kwanza nakubaliana na wazo lako, ila nadhani jina la Michuzi linanafasi yake kwan ndio mdau mkubwa, na pili kwanini unatumia kingereza? Kama nikubadilisha jina tutafute jina la kiswahili vinginevyo sioni mantiki yakulibadili hilo jina.
ReplyDeleteAcha hizo mazee, jina la ISSAMICHUZI.BLOGSPOT.COM (a.k.a GLOBU YA JAMII) ni jina kubwa, kwa lugha ya kimombo ni 'BRAND' kama vile CNN, Aljazera, BBC n.k hivyo wazo lako la kubadilisha jina iwe 'GLOBAL BLOG' a.k.a GB11, halikubaliki.
ReplyDeleteNi sawa BRAND ya JOHN WALKER WHISKY au VODKA useme unataka kuzibadilisha majina sidhani kama wadau wa brand hiyo watakuelewa.
Labda wewe JUNIOR uanzishe blogu yako kwa jina GLOBAL BLOG tuone kama ni jambo dogo kujijengea 'BRAND'.
Mwisho ISSAMICHUZI.BLOGSPOT.COM a.k.a GLOBU YA JAMII IDUMU!
Ni kweli naona tubadilishe jina Global Blog ila swala la kubadili mwaka kila mwaka unavyobadilika siafikiani nalo kama tutaweka mwaka basi usibadilike.
ReplyDeleteNGUMU, NI NGUMU SANA HII KUBADILI JINA HILI TUKUMBUKE KUWA JINA LA MICHUZI BLOG SASA LIMESHAKUWA NA NAFASI YAKE KUBWA TENA... NAONGEA HIVI KWA SABABU HATA LEO HII UKIENDA KUSEARCH KWA SEARCH ENGINE YOYOTE NIKIMAANISHA GOOGLE,BING,YAHOO NA ZENGINE ZOTE UZIJUAZO UKIANDIKA TUU MICH.... HATA HAUJAMALIZA LIBENEKE LINAJITOKEZA HAPO, NAMBA MBILI JINA LAKO ULILO SAJEST MKUU HALINA UBUNIFU WALA UHALISIA KABISA,LIKIWA HIVYO TUTALIANGUSHA LIBENEKE LA JAMII KABISA, NASEMA HIVI NIKIMAANISHA HIYO GLOBAL NI JINA COMMON SANA HALINA UPEKEE NAWEZA SEMA HIVYO KWA MAANA HIYO UNGEKUJA NA JINA BORA ZAIDI JINA NAONA HALIKUBALIKI NA PIA KUBADILISHA SIJUI KILA MWAKA HIYO NDIO KABISA MIMI NASEMA PIA HAIWEZEKANI,MDAU UNA HOJA NZURI LAKINI KUMBUKA KUFANYA MABADIRIKO INACHUKUA MUDA WATU KUZOEA JINA, NAKUMBUKA LIBENEKE HILI LILIANZA NA WWW.MICHUZI.BLOGSPOT.COM LAKINI WAKAONA KUNA UMUHIMU WA KUBADILI JINA NA BAADA YA SIKU AMA MASAA KADHAA WAKABADILI JINA NA KUWA WWW.ISSAMICHUZI.BLOGSPOT.COM . NAISHIA HAPA KWA KUWA MIMI SIO MSEMAJI MKUU WA LIBENEKE LA JAMII NI MCHANGIA MAWAZO TUU KAMA TULIVYO OMBWA KUCHANGIA...
ReplyDeleteLIBENEKEEEEEEEEEE!!!!!! OYEEEEEEEEEEEEE!!!!! MICHUZI NA WANAOSABABISHA LIBENEKE LA GLOB YA JAMIII LIENDE LEEE HOYEEEEEEEEE!!!
MIAKA SITA YA LIBENEKE LA GLOB YA JAMIIIIIII HOYEEEEEEEEE
ALUTA KONTINUA ANKALI PIGA KAZI MPAKA MWISHO
NAMALIZA KWA KUSEMA BIG UP!!!!
Wewe mdau inabidi utuombe radhi kwa kutuletea wazo hili,wewe unafahamu uzito wa Michuzi katika anga za uandishi wa habari?Jina lake ndio linalobeba imani ya wasomaji,na hao watu wa mashariki ya kati wanaruhusiwa pia kutumia english bila ya kikwazo,umeshawahi kumuona Mashaka akiandika kiswahili?na mbona article zake are mostly interactive na wadau.
ReplyDeleteMdau USA
Mimi nadhani kubadilisha jina ni mwanzo wa kupoteza mwelekeo wa Globu ya jamii
ReplyDeleteJiulize ni watu wangapi wanaifahamu kwa jina hili ni mitandao mingapi inaifahamu kwa jina hili
Kitendo cha kubadilisha jina ni kuipotezea umaraafu na kupoteza wadau wengi na kuipunguzia sifa katika nyanja za kimataifa na pia ule umatumbi wetu utapotea kabisa.
pia kitendo cha kila mwaka kuitwa gb11, gb 12 haina maana kabisa
ikitokea voting ya long standing blog yetu itapoteza sifa so hakuna kubalisha
ankal ni nembo yetu so aluta continue.
NOOOOO big noooooo...Hayo ni mawazo yako na unaruhusiwa kuwa na mawazo lakini kwa upande wangu goodwill ya jina la michuzi ni kubwa sana...Mambo ya GB wala siyafagilii kabisa...Stick to your name Michuzi Blog motto blog ya jamii.
ReplyDeleteMImi the thing ningekuambia ni kuwa hizo heading zako hapo juu za biashara basi ungeweka na heading yako ili mtu akiwa nasoma blog yako au akiwa anaacha comment basi aweze kerudi direct kwenye blog yako au weka pop upya kuacha comment this way inasumbua kurudi nyuma na hakuna heading ya kuturudisha nyuma basi inagua vurugu tupu
ReplyDeletehakuna hiyo jina hili hili ndo linabamba dunia nzima hilo la global litafaa zaidi ukilitumia mwenyewe. mbona wewe tangu umezaliwa hujabadili jina? michuzi tafadhali sana usibadili jina la sasa tena lina mvuto na nyota kali
ReplyDeleteUkibadilisha tu jina NDIYO UMEJICHIMBIA KABURI...kuna kitu kinaitwa BRANDING, na ndiyo msingi wa mafanikio ktk biashara na kwasasa MICHUZI BLOG ndiyo brand DUNIA NZIMA...NIMEMALIZA...don't say i didnt warn you Michuzi
ReplyDeletekasumba ya huyu jamaa isipewe nafasi, GB kirefu chake ni good bullshit, je unataka tuitwe hivyo.
ReplyDeleteIbadilike jina iwe blog ya jamii. sioni mantiki ya jina kubadilika kila mwaka.
ReplyDeletehuyu jamaa kanichafua sana nusura ya kutapika yaani he !!! ngombe wengine bwana, eti tutaheshimiwa na kuthaminiwa tukibadili jina , please stop this nonsense, halafu acha kutusomesha hadith ndefuu ya maoni yako,so you believe in yourself ha !! kuna website inaitwa kijiji ni maarufu sana duniani na ni wazungu sana wanaitumia na neno kijiji wengi wao hawalijui,au neno safari -mpaka kuna magari yanatengenezwa na kuitwa safari- wewe vipi ndugu yangu,au umesoma sana !!! regards ni mimi wa magomeni
ReplyDeleteKwanza napenda kumpongeza mdau aliyeleta mawazo yake ya kubadili jina la blog. Lakini kw amtazamo wangu naona haitakuwa busara kuweka jina la kidhungu. Ni bora tutafute jina la kimatumbi ambalo linawakilisha utanzania halisi na jamii yetu. Haya majina ya kiingereza mimi siafikiani nayo. Itakuwa sawa na wanafilamu wa bongo kuipa jina la kizungu sinema huku ikiwa ni ya kiswahili.
ReplyDeleteHakuna kubadili jina wala nini. Sisi bado tuna imani na jina la sasa hivi
ReplyDeleteJina si kitu ubora kilichomo! Tuondokane na utamaduni wa majina bora... lolote lile ni jina ilimradi linamtambulisha mtu au kitu.
ReplyDeleteTumezoea michuzi ibake vile vile.
ReplyDeleteBadilisheni jina mnavyotaka ila neno MICHUZI liwemo(Biashara ya kubadilisha majina yaachie makampuni ya simu!!)..Wataalam wa Masuala ya Marketing watasaidia sana kwenye michango.Pliiz wadau wa Marketing
ReplyDeleteNi mimi David V
watanzania mbona mnapenda mambo ya kuiga iga tuuuuuuu ujinga mtupu wewe kama unaona jina hili halina soko anzisha la kwako,kipende kitu chenu,hivi kwani wenzetu wachina wanafanyaje mambo yao??sidhani wanapofanya mambo yao wanahitaji kuiga lugha ya mtu!!!kwanza nafikiri jina linawakilisha uhalisia wa mtu na asili yake sioni sababu yoyote ya msingi uliotoa eti kupata wadau wa kimataifa kujenga nchi yetu au kutoa mawazo yao kupitia blog hii sababu ya jina!!!kama wanataka kuchangia mada na wachangie sasa hivi kwa jina hili hili si lazima majina yawe ya lugha za wenzetu tu ndio mfahamike kimataifa,wakongo man wale pale na nyimbo zao za kikongo mbona wanauza kimataifa??tatizo sio jina labda tatizo wewe mwenyewe na kihelehele chako cha kutaka kujifanya unajua zaidi.kaanzishe blog yako uite jina hilo unalotaka halafu uone wangapi watakuja hao unaotaka kutoka nje,kwani leo miaka sita huko nyuma ilikuwaje na mpaka sasa iko vipi???nani kaifanya ifike hapa ilipo leo kama si wana libeneke wenyewe wabongo???naona mawazo yako na akili yako vimegandana na makamasi kwa kupenda vya watu.
ReplyDeletemdau LAS VEGAS,NEVADA
USA
Kwanza kabisa Hoja alizotoa mtoa mada mkuu ni faida za blog yoyote tu na sio faida za kubadili jina kama anavyodai. haviunganiki. No connection na hoja yake.
ReplyDeletePili suala la jina kubadili sina tatizo. Size ya michuzi blog ni kubwa na mimi nashauri jina jipya ambalo kila mtu atajiona ni part yake tofauti na sasa ambapo inaonekana kama ni blog ya mtu Live yaani Issa michuzi. Ni blog ya mtu ila sisi tunakutana tu kuchat then tunaondoka. Toa jina neutral kama zinavyoafanya blog kubwa za hapa bongo na ulimwenguni. eg nyumbani. jamvini, kijiweni. A neutral name.
Nawasilisha.
TROUBLES WITH CHANGING A BRAND NAME
ReplyDeleteBranding “involves decisions that establish an identity for a product with the goal of distinguishing it from competitors.” Because this is the goal companies have been known to spend huge amounts on research to come up with the perfect name for their product. But coming up with a name for a brand can be tricky. There are many things that must be taken into consideration including what the name evokes in the minds of customers.
According to this rebranding proposal, ‘issamichuzi’ as a brand name may be facing a problem with what their brand means to customers. Not the ‘issamichuzi’ name but their new brand name – ‘Global Blog’. Remember this: What does ‘Global Blog’ conjure in the minds of consumers? Well that remains to be seen but this rebranding proposal suggests that ‘issamichuzi’ may initially face a ‘rough ride’ with the new name. It's a complete and total waste of time and resources.
WHEN TO CHANGE YOUR BRAND NAME
“The sweetest word in the brand universe is your brand’s name.” This obvious quote is from Bill Schley & Carl Nichols, Jr. in their unheralded book “Why Johnny Can’t Brand.”
Your name is the first and most powerful part of your brand. A great name can help you stand out in a crowded market. It can position you as a leader, convey your culture, even explain what you do in a word or two.
Conversely, a weak name can neutralize or even negate the work you do to build a brand and market position. A weak name is easily forgotten and can limit your opportunities in other markets if you plan to expand.
Consumer product companies understand this, and tie their brand names directly to their brand strategies. Most B2B companies take a more haphazard approach. Those that don’t put any effort into branding simply choose a name, charge forward and end up being “branded” by the market. Or worse yet, they’re simply ignored.
It’s a big undertaking to change your brand name. When is it worth it? Consider changing your name if you’re redefining or repositioning your brand. Here are three reasons to do it:
1. Change to distance yourself from a negative event.
2. Clarify a confusing or non-descript brand.
3. Better represent an upgraded product/service that’s outgrown the existing brand
4. ‘issamichuzi’ may decide to rebrand if and only if its core services have changed, as a revenue buster, etc.
My verdict: ‘issamichuzi.blogspot.com’ should stay put, PLEASE!!
Mdau Mwita wa Kibumaye Tarime
IssaMichuzi ndiyo identity yako.
ReplyDeleteKatu usijaribu kubadilisha jina.
Hapo lilipo imechukua miaka sita kulijenga.
IssaMichuzi to stay plz
Nashukuru wadau kwa mawazo na mtizamo wenu kuhusu Blog yetu hii ya jamii. Mimi kama mdau mkubwa wa Blog hii ya jamii sioni haja ya kubadili jina, tena ati liwe linabadilika kila mwaka, kwanini yote hayo? Jina la Michuzi lina umuhimu wake katika Blog hii nadhani ni vizuri lisiachwe. Muhimu kama ni kubadili basi labda iwe kwenye habari zenyewe, namna zinavyoandikwa. Nawasilisha.
ReplyDeleteMawazo yako yanaheshimiwa. Ingawa mimi binafsi sikubaliani nayo. Blog hii ya jamii iendelee kuitwa MICHUZI BLOG. Hii ndiyo blog ya kwanza kuchukua nafasi ya kimataifa hapa Tanzania na hivyo basi historia yake inatakiwa itunzwe. Kubadilisha jina ni kuifuta historia ya Blog yetu.
ReplyDeleteANKAL MICHUZI KWELI WEWE MDEMOKRASIA. NINGEKUWA MIMI WAZO HILO NISINGELICHAPISHA KABISA KTK BLOGU. KWA KIFUPI HATUIHITAJI JINA JINGINE ZAIDI YA MICHUZI BLOGU LINAONYESHA UASISI NA PIA NI TRADEMARK AU SIJUI BRAND NAME. LEO TUTAIBUKA KUSEMA KWASABABU NOKIA ZINATUMIWA NA KUPENDWA NA WATU WENGI PENGINE TUZIITE GLOBAL PHONE ...AU TOYOTA NI MAARUFU BASI TUIOBADILI KUWA GLOBAL CAR 2011 ... NO WAY!!!.
ReplyDeleteANKAL UMEPEWA WAZO TUTATOA MAWAZO YETU PENGINE YA KUBADILI JINA YATAKUWA MENGI KULIKO YA SISI TUSIOTAKA MABADILIKO... BASI AKILI ZA KUAMBIWA............(MBAYUWAYU CASE).
ASANTE MTOA WAZO UMETOA MAWAZO YAKO YAHESHIMIWE.
MDAU
Jina la Issamichuzi limetamalaki kila kona ya dunia. Ni BRAND kubwa ambayo kuibadili ni kurudi nyuma. Haya mambo ya "global something" yako mengi naona kama tuyaache yaliyopo yawe hayo hayo. Issamichuzi aka globu ya jamii idumu daima dumu amin!
ReplyDeleteHuyu aliyetoa wazo hili ni lazima atakuwa amesoma sana, na pia jina lake kamili ni lazima litakuwa Stewart Arthur Davidson McFarland.
ReplyDeleteMICHUZI SIKU UTAKAYOBADILISHA JINA LA BLOG YA JAMII NDIYO SIKU UTAKAPOKUWA UMEPOTEZA MDAU MMOJA TUU, NA HUYO MDAU NI MIMI.
mimi nawapongeza wote waliokataa kubadili jina la blog yetu ya jamii kwani mimi na mjua michuzi tangu daily news mpaka leo amekua mwana blog sasa ukibadili jina uta haribu maana ya ISSA MICHUZI.duniani kote
ReplyDeletesays Derick mshana
hili wazo halikubaliki kabisaaaaa!!
ReplyDeleteNOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO KAMA ANAONA HALIFAI AANZISHE GLOBU YAKE LIBENE OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
ReplyDeleteMZEE WA BUNJU
JK junior sio mdau kama anavyojiita, ila ni mmoja wa wale wale, wanaijeria. Safari hii tumekustukieni MAPEMAAAAA. bye.
ReplyDeleteMichuzi liko juu, hamna cha kubadilika wala nini, hata akifa basi mrithi ni lazima akeep hili jina unless otherwise, litote tugawane mbao
ReplyDeleteYANI UKIBADILI HILO JINA NA WEWEW UJITOE KABISA KWENYE LIBENEKA HATUTAKI MAWAZO MGANDO SISI, WE MTOA MADA UNATAKA BLOG YRTU IWE KAMA HIZO HOTELI ZENU MNAZOBADILI MAJINA KILA SIKU?????????? NASEMA HATUTAKIIIIIIIII HUSIKIIIIIIIIIII ALAAAAAAAAAAAAAAAAH!
ReplyDeleteMichuzi isibadilike, hata asipokuwepo Issa, lakini kumbukumbu ya kitu kizuri alichoanzisha itakuwepo. Nashauri jina libaki kama lilivyo. Labda neno ISSA linaweza kupunguzwa likabaki www.michuzi.blogspot.com
ReplyDeleteMdau wa Blog ya Jamii, UK
Mimi nashangaa! watu wengine wanatoa maoni kama wanagombana au kama wananjaa hivyo wanalazimishwa kutoa maoni.Kama huoni inafaa si utumie lugha ya kiistaarabu tu hadi matusi dah,wadau bana!
ReplyDeleteMdau washukuriwa kwa wazo lako
ReplyDeleteIsipokuwa ni bora zaidi jina liendelee kubaki hili hili
kutokana na umaarufu wake na kwa kuwa jina hili lawakirisha kimatumbi.
Ningekubaliana nawe japo kidogo iwapo kama wazo la jina lako lingekuwa ni la kimatumbi. Ama jina la kizungu sipendezewi nalo ni lazima nasi tujivunie lugha yetu na utamaduni wetu.
Kwa majumuisho, waliosema HAPANA wameshinda na waliosema ndiyo jina libadilike wameshindwa. Kwa hiyo jina litabaki lilelile MICHUZI BLOG.
ReplyDeleteWAZO LAKO MDAU SIO BAYA ILA KUBADILI BRAND NAME AMBAYO IMESHAKUBALIKA SI KITU CHA BUSARA..MFANO MZURI NI KAMA LEO UMWAMBIE STEVE JOBS ABADILI JINA LA APPLE COMPUTERS NA KUITA GLOBAL COMPUTERS ETI KWA SABABU INAUZA DUNIA NZIMA..MICHUZI MI NAONA NI BRAND AMBAYO IMESHAJIJENGA TAYARI NA INAKUWA..KUIBADILI LEO HII SIONI KAMA NI JAMBO LA BUSARA..ASANTE
ReplyDeleteHakuna kubadilika kitu humu ndani, kuanzia 'globu yetu', lugha yetu ya chuo kikuu cha university na maihazbend na mtaa wa street! Msitufanye wanalibeneke tuende Tahrir Square pale Mnazi Mmoja kudai brand ya Ankal Misupu ibaki palepale kama ilivyo!
ReplyDeleteNimefunga mjadala Ankal! Maoni zaidi wadau pelekeni SMS 911 (sijui tunayo?)
Michuzi inatisha....hakuna kubadilisha wala nini wala sio kweli kwamba ukibadilisha jina ndio utaipa sura ya kimataifa hapa ilipo tayari inaangaliwa kila mahali....Libeneke Oyeeeeeeeeeeee..
ReplyDelete