KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo ametangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena.

Mchezaji aliyeitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Mwandini Ally wa Azam huku pia akimjumuisha kwenye kikosi chake mshambuliaji wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Thomas Ulimwengu.

Kikosi kamili ni makipa Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya), Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Godfrey Taita (Yanga) na Juma Jabu (Simba).

Viungo ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Ramadhan Chombo (Azam) na Shomari Kapombe (Simba).

Washambuliaji katika kikosi hicho ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), Hussein Javu (Mtibwa Sugar) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).

Timu itaingia kambini Novemba 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 9 mwaka huu kwenda N’Djamena kwa ajili ya mechi hiyo. Stars na Chad zitarudiana Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Powered by Sorecson : Creation de site internet

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. nimefurahi wachezaji wa Simba 5 na wachezaji wa yanga 3.

    ReplyDelete
  2. Tunahitaji zaidi vijana na bahadhi ya wakubwa wachache ambao wanafahamika michango wao kwenye timu ya Taifa...Poulsen hajiamini.Hatuhitaji wazee sana kwa sasa..hii timu ndiyo ileshindwa kutupleleka Equatorial

    David V

    ReplyDelete
  3. Tatizo letu ni kwamba kila mara tunaweka timu kambini kufanya mazoezi ya pamoja kwa muda wa siku 7 tu!! Vipi, hatuna hela? Hili tu ni mojawapo ya sababu zinazosababisha tusifanye vyema. Mimi ninazo nyingi! Tunaitakia timu yetu vyema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...