Na Waandishi wetu

Kikundi cha kigaidi cha Al-Shaabab kimezua hofu kuelekea kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya Simba na Yanga kesho baada ya Jeshi la Polisi nchini kutoa taarifa ya kuzuia mikusanyiko kwa kuwa wana taarifa kwamba kikundi hicho kina mpango wa kufanya mashambulizi jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa wamezuia maandamano yaliyokuwa yafanyike kesho ya Mtandao wa Wanaharakati ya kupinga Serikali kuilipa kampuni ya umeme ya Dowans kwa kuwa Jeshi la Polisi nchini limepata taarifa kuwa kikundi hicho cha kigaidi kinapanga kufanya mashambulizi kwenye mikusanyiko ya watu jijini Dar es Salaam.

"Hatuwezi kuruhusu maandamano ya aina yoyote wala mikusanyiko mikubwa kwa njia ya mikutano ya hadhara hivyo maandamano yaliyokusudiwa na taasisi hizo yanasitishwa kwa sababu za kiusalama nilizozitaja," alisema Kova.

Hata hivyo, Kamanda Kova aliwataka mashabiki kufika kwa wingi katika mechi ya Simba na Yanga kushangilia timu zao kwa sababu uwanjani hapo kutakuwa na ulinzi wa uhakika na hata hivyo "Al Shabaab wanapenda kwenye mikusanyiko ya wanaharakati."

Kova alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, wamepanga mkakati madhubuti kuhakikisha kwamba mchezo huo unafanyika kwa amani na utulivu.

Kova alisema kiwango cha usalama na utulivu kilichokusudiwa kitamwezesha shabiki au mpenzi wa soka kwenda uwanjani na kuondoka kwa usalama, yeye pamoja na familia yake.

Alisema Jeshi la Polisi limechukua hatua madhubuti za kiulinzi na kiusalama, ambazo ni pamoja na kutoruhusiwa mtu yeyeyote kuingia na kilevi chochote uwanjani au kunywa kinywaji chochote chenye kilevi.

Alisema watu hawaruhusiwi kubeba silaha ya aina yeyote uwanjani kama vile kisu, panga na kadhalika na kwamba mashabiki hawaruhusiwi kuhama au kuvamia majukwaa ambayo ni tofauti na gharama za tiketi zao.

Alisema Jeshi la Polisi litaweka kamera maalum za video ili kuweka kumbukumbu na kubaini matukio yote yatakayojitokeza uwanjani kabla na baada ya mchezo huo na pia utupaji wa chupa zenye kimiminika cha aina yeyote hauruhusiwi na haivumiliki na hatua dhidi ya vitendo hivyo zitachukuliwa.

Vilevile alisema wale wote watakaobainika na makosa ya uhalifu, majina yao yatatangazwa pamoja na picha zao kuonyeshwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa lengo la kukomesha tabia mbaya za kihuni.

Alisema shabiki yeyote atakavamia "dimbani" wakati wa mpira ukichezwa kwa sababu anazozijua mwenyewe, atapigwa picha, alama za vidole na kumbukumbu zote muhimu zitachukuliwa na atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka.

Kova alisema mtu yeyote atakaeona kitendo cha uhalifu uwanjani hapo, atume ujumbe mfupi wa (sms) kwenye namba 0783034224, ambapo ujumbe huo utaingia katika kompyuta ya polisi itakayokuwepo uwanjani hapo na hatua zitachukuliwa mara moja.

Shirikisho la Soka nchini (TFF) kupitia kwa katibu mkuu wake Angetile Osiah lilisema jana kuwa halikuwa na taarifa juu ya tishio la Al-Shabaab kushambulia jijini Dar es Salaam kama ilivyoelezwa na Jeshi la Polisi lakini wanalifanyia kazi.

"Hatuna taarifa zozote, lakini kesho kutakuwa na kikao cha wadau wote wa mechi ya Jumamosi (kesho) hivyo tutajadili suala la hilo ili kuona tunachukua tahadhari zipi," alisema Osiah.

Alisema kuwa kikao hicho cha leo mbali na kuwahusisha viongozi wa Simba na Yanga, pia kitalishirikisha Jeshi la Polisi pamoja na maafisa wa Usalama wa Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Jambalaya med risOctober 28, 2011

    YAAN mkuu anatufanya watoto wadongo bomu linalolipuka watu wakiwa wamefungamana na bomu la wazi lipi linaasili kubwa kwli kwenda shule cio kuelewa mambo yote kwenye maisha aaaya mkubwa inabidi tukubali tu cc wanyoge kila siku

    ReplyDelete
  2. Taarifa hii irudiwe mara moja ili tuelezwe mambo ya maana. Upande mmoja inaongelea hatari ya shamulio la kigaidi, na upande wa pili limesheheni ufafanuzi wa kile mashabiki wasichopaswa kufanya wawapo uwanjani (kitu ambacho hakihusiani na ugaidi bali uvunjaji wa amani mchezoni, hali ambayo haimbatani wala kuhusiana na ugaidi). Maana ya hii taarifa ni nini? Tupewe taarifa ya kujihadhari na ugaidi na isichanganywe na taarifa zingine. Ya ugaidi ni nyeti sana, usiichanganye changanye wala kuitilia siasa siasa. Makosa ya vyombo vyetu vya dola ndio huwa yanaanza hivi hivi.

    ReplyDelete
  3. Du! Hii kali. Sasa siasa za uongo zinaingia Tanzania! Nadhani lengo ni kuzuia maandamano na si magaidi hawa. Mimi hapa sina mbavu. Hii ni kama maoka!

    ReplyDelete
  4. Hawana chochote wanaogopa maandamano tu

    ReplyDelete
  5. Hii habari mbona haina kichwa wala miguu.Huyo kova kalewa nini Al-shabab washambulie Dar kwa sababu zipi? Acheni kuchezea akili za watu na msiwanye watu wajinga.Shabab sio vichaa walipue sehemu bila sababu na km issue ni kulipuliwa kwa Kenya nikwa sababu majeshi ya Kenya yameingia Somalia.Huyo Kova atafute jambo jengine lakuwakataza hao wanaotaka kuandamana lakini asiseme 7bu ni Al-shabab.Me nashangaa sana mtu mwenye cheo kama Kova anongea pumba namna hii,anatoa madai bila ufafanuzi na kwataarifa yako kova Shabab wakitaka kulipua wala hamtaweza kuzuia bcoz hamna uwezo polisi wa bongo mnachoweza ni rushwa tu.

    ReplyDelete
  6. Akya nani Kova nimekuvulia kofia; kwenye maandamani mnatishia Al Shabab; kwenye mechi ambayo ni uwanja ambao umezungushiwa uzia (meaning ni hatari zaidi) usalama upo. Umetumia akili sana kuwa stopisha waandamanaji.. Aaaah

    ReplyDelete
  7. Wabongo wengine kweli mmezoea sana amani kukiwa na fununu za mambo ya kiusalama kwa siye wanausalama lazima tuchukue taathari. tusipofanya hivyo baadaye mtakuja tuu kutulalamikia, habari ndo hiyo kila mtu awe macho

    ReplyDelete
  8. Doo mbona balaa,propaganda za kimarekani sasa zinafanya kazi bongo,mambo mazuri.

    ReplyDelete
  9. mwisho wa dunia kila mtu atasema lake,nadhani yatupasa kuwa makini sana nyakati hizi,pili ni bora mungu aje kwa namna yoyote ile hata kwa gharika ili akifute hiki kizazi ni hayo tu amina.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...