Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la mauwa kwenye Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere baada ya misa maalum ya kumkumbuka muasisi huyo Taifa la Tanzania iliyofanyika leo kijijini kwake Mwitongo Butiama. |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzinduwa kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza iliyoambatana na maadhimisho ya miaka 50 Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika jana katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mara. Kulia Waziri wa Habari utamaduni na Michezo Mhe. Dkt Emanuel Nchimbi na kushoto ni Naibu waziri katika wizara hiyo Dkt Fenella Mukangara
Mwandishi wa Habari na mpiga picha mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo Bi. Anna Itenda, kwa niaba ya waandishi wa habari wa Tanzania, akiweka shada la mauwa katika kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalim Julius Nyerere wakati wa misa maalum ya kumkumbuka muasisi wa Taifa la Tanzania iliyofanyika jana kijijini Mwintongo Butiama. |
Picha zote na Amour Nassor wa VPO
bilal unajua maana ya mwenge?nahisi huijui ungeijua usingefanya ulivyofaha hapo pichani au kwa vile unataka raha ya dunia
ReplyDelete