Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa uhuru kiongozi wa mbia za mwenge huo mwaka 2011 2012 Mtumwa Rashid Halfan kutoka mkoa wa kaskazini Unguja, kwa ajili ya kuanza mbio za kukimbiza katika mikoa yote ua Tanzania baada ya kuuwasha rasmi leo katika kijiji cha Butiama Mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la mauwa kwenye Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere baada ya misa maalum ya kumkumbuka muasisi huyo Taifa la Tanzania iliyofanyika leo kijijini kwake Mwitongo Butiama.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzinduwa kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza iliyoambatana na maadhimisho ya miaka 50 Uhuru  wa Tanzania Bara zilizofanyika jana katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mara. Kulia Waziri wa Habari utamaduni na Michezo Mhe. Dkt Emanuel Nchimbi na kushoto ni Naibu waziri katika wizara hiyo Dkt Fenella Mukangara





Mwandishi wa Habari na mpiga picha mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo  Bi. Anna Itenda,  kwa niaba ya waandishi wa habari wa Tanzania,  akiweka shada la  mauwa katika kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalim Julius Nyerere wakati wa misa maalum ya kumkumbuka muasisi wa Taifa la Tanzania iliyofanyika jana kijijini Mwintongo Butiama. 

 Picha zote na Amour Nassor  wa VPO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. bilal unajua maana ya mwenge?nahisi huijui ungeijua usingefanya ulivyofaha hapo pichani au kwa vile unataka raha ya dunia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...