Zana za milipuko ya kuulia samaki iliyokamatwa katika kijiji cha Somanga wilayani Kilwa kufuatia taarifa ya wasamaria wema wanaopenda kutunza raslimali za bahari
.Mwenyekiti wa  kikosi cha Doria BMU Somanga ,Mohamed Ibrahim akiwaonyesha baadhi ya maofisa uvuvi wilayani Kilwa milipuko iliyokamatwa na kikosi chake baada ya watuhumiwa kufanikiwa kukimbia


Picha na habari na
Abdulaziz Video, Lindi


Kikundi shirikishi cha Usimamizi wa Rasilimali za Pwani na Bahari cha kijiji cha Somanga (BMU) Wilayani Kilwa Kimefanikiwa kukamata Milipuko kumi,vibati 8 na Utambi wa kulipulia futi mbili baada ya Wahusika wa
milipuko hiyo kufanikiwa kutoroka baada ya kuhisi kufuatiliwa na kikundi hicho

Akiongea na Globu ya Jamii baada ya kukamata Milipuko hiyo,Mwenyekiti wa Doria BMU Somanga,Bw Mohamed Ibrahim alieleza kuwa kikundi hicho kwa kushirikiana na Polisi jamii waliletewa taarifa kwa njia ya simu
na raia mwema na walipofuatilia watuhumiwa walikimbia na kuacha milipuko hiyo iliyofikishwa kituo cha Polisi Wilayani Kilwa. Mlipuko mmoja ilibidi kulipuliwa na jeshi hilo kutokana na kuwa katika hali ya Hatari

Nae Afisa Maliasili na Mazingira Wilayani Kilwa, Bw Raymond Ndumbalo, licha ya kupongeza kazi nzuri ya BMU Somanga Kwa kufanikiwa kukamata mara kwa mara zana haramu za uvuvi amesema ni Vema jamii ikashirikina  na kufanya kazi pamoja na serikali ili kumaliza tatizo hilo 



Aidha Ndumbalo licha ya kueleza tatizo hilo la milipuko amesema tatizo lingine wilayani Kilwa ni pamoja na uvuvi wa kutumia nyavu zenye matundu madogo pamoja na sumu.


Mmoja wa mamiliki wa vyombo vya Uvuvi wilayani humo,Bw Ahmaid Shukra na Mohamed Nalinga waliotoka kuvua kwa pamoja  walieleza kuwa wila ya kuboresha wavuvi wilayani Kilwa Uvuvi haramu hautomalizika kutokana na wavuvi wengi kuwa duni kimaisha. Walieleza sababu zinazochangia kuwepo kwa matukio hayo yanayofanywa na wananchi kutoka maeneo ya nje ya kijiji hicho na wale wenyeji ni kutokana na kukosa zana bora zinazokubalika kisheria

Uhifadhi wa Raslimali za Pwani na Bahari ni moja ya mipango inayolenga kutunza rasilimali hizo huku kijiji cha Somanga kikiongoza kwa matumizi ya zana haramu zikiwemo nyavu zenye matundu madogo, (kokoro),Baruti pamoja na sumu kuua samaki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...